Home Kitaifa MPANGO KAZI WA KITAIFA KUKOMESHA MAUAJI YA WENYE UALBINO WAPOGEZWA NA WADAU

MPANGO KAZI WA KITAIFA KUKOMESHA MAUAJI YA WENYE UALBINO WAPOGEZWA NA WADAU

Na Hamida Ramadhan, Dodoma

WADAU mbalimbali wamejitokeza kupongeza hatua ya serikali kuzindua Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki na Ustawi kwa Watu Wenye Ualbino, wakisisitiza kuwa kama utatekelezwa ipasavyo, utasaidia kukomesha mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya FDH inayojihusisha na masuala ya watu wenye ulemavu mkoani Dodoma, Maiko Salali, alisema hayo hivi karibuni wakati wa kutoa tamko la kuipongeza serikali kwa kufanikisha mpango huo muhimu.

“Ni imani yetu kuwa mara baada ya kuzinduliwa kwa mpango huu, changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili watu wenye ualbino nchini zitapatiwa suluhisho, na kundi hili litaweza kufurahia maisha yao ndani ya taifa sawa na wananchi wengine,” alisema Salali.

Alibainisha kuwa watu wenye ualbino wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo mitazamo hasi kutoka kwa jamii. Alisema mitazamo hiyo potofu imekuwa chanzo cha madhila makubwa, ikiwemo mauaji, kukatwa viungo, na ukatili wa aina nyingine.

“Hivyo, ni matarajio yetu kuwa kama mpango kazi huu wa kitaifa wa haki na ustawi kwa watu wenye ualbino utasimamiwa vizuri na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, tutafanikisha kukomesha mauaji ya kundi hili,” aliongeza Salali.

Aidha, alisema mpango huo pia utapunguza matukio mengine ya kikatili, kama vile kukatwa viungo kwa wenye ualbino, jambo ambalo limekuwa likishuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kutokana na imani potofu za kishirikina.

Kadhalika, Salali alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali kwa kufanikisha mpango huo muhimu kwa ustawi wa watu wenye ualbino na taifa kwa ujumla.

“Napenda kutumia fursa hii kwa mara nyingine, kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kupitia ofisi yake, ambayo imeratibu na kufanikisha mpango kazi huu. Aidha, tunampongeza sana Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, kwa kuongoza mchakato wote wa kufanikisha mpango huu kupitia kitengo cha watu wenye ulemavu kilichopo chini ya ofisi yake,” alisema.

Pia, Salali aliwashukuru wadau wote waliosaidia kufanikisha mpango huo, wakiwemo Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS), Standing Voice, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), na wengine ambao walitoa mchango wao wa rasilimali, fedha, na mawazo.

Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki na Ustawi kwa Watu Wenye Ualbino ulizinduliwa tarehe 3 Desemba 2024, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!