Home Kitaifa GENERATION SAMIA YAATHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU KWA KUFANYA USAFI DODOMA

GENERATION SAMIA YAATHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU KWA KUFANYA USAFI DODOMA

Na Hamida Ramadhan, Dodoma

Dodoma, Desemba 9 – Kundi la vijana wa Generation Samia (Gen S), linalojulikana kama “Kizazi cha Mafanikio,” limeadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa Gen S, Sonatha Nduka, amesema wanashukuru serikali kwa kuwawezesha kushiriki shughuli za kijamii kama njia ya kuwaenzi waasisi wa taifa.

“Tunatekeleza kwa vitendo maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kushiriki katika shughuli za kijamii, kama kutunza mazingira na kutumia nishati safi ya kupikia,” alisema Nduka.

Aidha, alibainisha kuwa Gen S pia inahamasisha uchangiaji damu na inajipanga kuanzisha tukio kubwa litakalohusisha wahitimu wa elimu ya juu kujadili namna ya kutumia fursa za kujiajiri.

Kwa upande wake, Kiongozi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Paul Julius Mageni, amepongeza juhudi za Gen S kwa kutambua umuhimu wa mazingira safi kwa afya ya wagonjwa.

“Mazingira mazuri ni sehemu ya tiba. Tunawashukuru kwa mshikamano huu ambao unatoa mfano bora kwa jamii nzima,” alisema Mageni.

Gen S imesisitiza dhamira yake ya kuunga mkono ajenda za serikali, hasa katika suala la utunzaji wa mazingira kwa lengo la kulinda afya ya wananchi na kupunguza magonjwa ya mlipuko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!