Home Kitaifa TRA YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA MAADILI YA WATUMISHI WAKE

TRA YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA MAADILI YA WATUMISHI WAKE

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salumu ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa jitihada zake za kuimarisha maadili kwa watumishi wake, akieleza kuwa maadili ni msingi muhimu wa utendaji bora na utoaji wa huduma kwa walipakodi.

Sheikh Salumu amesema hayo leo, Mei 13, 2026, jijini Dar es Salaam alipokutana na watumishi wa Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa lengo la kujadiliana namna taasisi za dini zinavyoweza kushiriki katika kuimarisha maadili ya watendaji ndani ya mamlaka hiyo.

Aidha, viongozi wa dini wamempongeza Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Juma Mwenda kwa kutambua mchango wa taasisi za dini katika kujenga jamii yenye maadili, uadilifu na uwajibikaji. Wamesema ushirikiano huo utaongeza ufanisi wa TRA katika kuwahudumia walipakodi kwa kuzingatia sheria na misingi ya haki.

Kwa upande wake, Meneja wa Maadili wa TRA, Sospeter Makubi amewashukuru viongozi wa JMAT kwa kukubali kushirikiana na TRA katika kuimarisha maadili kwa watumishi wake, hatua ambayo alisema itasaidia kuongeza uaminifu kati ya TRA na walipakodi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!