Home Kitaifa KUSUASUA KWA MRADI WA AFYA DKT MAGEMBE ASHUSHA NONDO KWA WASIMAMIZI

KUSUASUA KWA MRADI WA AFYA DKT MAGEMBE ASHUSHA NONDO KWA WASIMAMIZI

OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Dkt. Grace Magembe ameagiza kufanyika Uchunguzi wa kina katika miradi yote nchi inayoonekana kuwa na Mapungufu na yeyote atakayebainika ni kwazo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake

Hayo ameyasema katika ziara yake ya kukagua Ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma ya afya katika hospitali ya Wilaya ya Kinyonga,kituo cha afya Hoteli tatu pamoja na Kipindimbi Zilizopo halmashauri ya Kilwa ambapo amedai hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Niseme Ofisi ya Rais- TAMISEMI itafanya uchunguzi wa kina katika miradi ambayo imeonekana kuwa na mapungufu na yoyote atakayebainika kurudisha nyuma utekelezaji huo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria za utumishi wa umma”amesema Dkt Grace

Dkt Magembe amesema Lengo la Serikali ni kuhakikisha dhidi isha wananchi wanapata huduma bora za afya, kutokamilisha miradi kwa wakati ni kwenda kinyume na azma ya Serikali ya awamu ya sita ya kumsogezea mwananchi huduma bora

Aidha pamoja na ucheleshwaji huo , Dkt. Magembe ameitaka Halmashauri ya Kilwa kuzingatia maelekezo na maagizo yanayotolewa na Serikali katika utekelezaji wa miradi hasa katika matumizi ya fedha ili fedha hizo zitumike kama ilivyopangwa na Serikali .

“ Ukiangalia Kituo cha Afya Kipindimbi Mil. 250 zilitakiwa zijenge jengo la wagonjwa wa nje, maabara pamoja na kichomea taka lakini kichomea taka hakijajengwa na fedha zimeisha. Hapa Hoteli tatu kichomea taka hakijajengwa, uchunguzi utakaofanyika utatuambia kwa nini mmeshindwa kutekeleza miradi hii kama Serikali ilivyoelekeza “ Dkt. Magembe

Pamoja na hayo Dkt. Magembe amewapongeza wananchi wa maeneo ya miradi kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuimarisha ulinzi na usimamizi wa miradi pamoja na kuchangia nguvu kazi katika utekelezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!