Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako leo tarehe 25 Jula, 2022, amekutana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika masuala ya Kazi, Vijana, na Ajira.
Waziri Ndalichako amemuhakikishia Balozi huyo kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana naye na ameomba kuwepo na Programu ya kuwausisha Vijana na masuala ya digitali ili waweze kutumia teknolojia kwa tija.
Naye, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot amesema Uswisi iko tayari kushirikiana na Ofisi hiyo katika kuleta Maendeleo kwa Vijana hususan kupitia Programu zao za Mafunzo ya Uanagenzi.
Viongozi hao wamekutana na kufanya mazungumzo hayo kwenye ofisi ndogo za Ofisi hiyo jijini Dar es Salaam.