Home Michezo KATIBU CCM WILAYA YA MUSOMA MJINI APONGEZA MASHINDANO YA MATHAYO CUP ,4...

KATIBU CCM WILAYA YA MUSOMA MJINI APONGEZA MASHINDANO YA MATHAYO CUP ,4 ZAFUZU NUSU FAINALI

Na Shomari Binda-Musoma

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma mjini, Burhani Buta amepongeza mashindano ya Mathayo Cup yanayoendelea kwenye uwanja wa shule ya sekondari Mara.

Burhani pia amezipongeza timu 4 ambazo zimefuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo yaliyozishirikisha timu 16 kutoka jimbo la Musoma mjini.

Akizungumza na Mzawa Blog wakati akifatilia mashindano hayo amesema ilani ya CCM inatekelezeka kwa asilimia 100 kwenye sekta ya michezo jimbo la Musoma mjini.

Amesema vijana wengi wameshiriki mashindano hayo kwa kucheza na kuyafatilia na ndivyo ilani inavyoelekeza.

Burhani amempongeza mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kwa kuandaa mashindano hayo kila mwaka.

“Mashindano haya yamekuwa na mvuto mkubwa na kuwavutia watu wengi na hili ni jambo kubwa kwenye jimbo letu la Musoma mjini”

“Tunampongeza mheshimiwa Mathayo kwa kufanya utekelezaji wa vitendo wa ilani ya uchaguzi ya CCM kupitia michezo” ,amesema Burhani.

Aidha katibu huyo amezitaka timu zinazoshiriki mashindano hayo kuendelea kudumisha nidhamu hadi mwisho wa mashindano.

Timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni pamoja Nyakato, Nyamatare, Mwigobero.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!