Home Afya WIZARA YA AFYA YAKUSANYA BILIONI 593 NDANI YA MIEZI TISA

WIZARA YA AFYA YAKUSANYA BILIONI 593 NDANI YA MIEZI TISA

TRILIONI 1.11 ZAPOKELEWA KUTEKELEZA MIRADI YA AFYA

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo, Jumatatu, Mei 11, 2026.

Katika wasilisho lake, Waziri amebainisha kuwa wizara imefanikiwa kukusanya asilimia 72.42 ya lengo lake la mapato ya ndani kufikia Machi 2026, huku akisisitiza kuwa utekelezaji huo unazingatia Ilani ya CCM ya mwaka 2025 na Dira ya Taifa 2050.

Waziri Mchengerwa ametoa mchanganuo wa fedha za wizara kwa kipindi cha kuanzia Julai 2025 hadi Machi 2026 ambayo Makadirio ya Mapato ya Ndani NI hilingi Bilioni 819.98, kiasi kilichokusanywa ni Shilingi bilioni 593.5 (72.42% ya lengo).

Waziri amewashukuru wadau wa kimataifa na kikanda kwa kuendelea kufadhili sekta ya afya nchini. Fedha kutoka mashirika kama Global Fund, Gavi, Benki ya Dunia, UNICEF, na UNFPA zimeelekezwa kwenye maeneo ya kimkakati kama mapambano dhidi ya UKIMWI, TB, na Malaria, uimarishaji wa huduma za chanjo na lishe, upatikanaji wa damu salama na kuboresha afya ya mama na mtoto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!