Home Kitaifa WAJASILIAMALI ZAIDI YA 1000 WAMEPATIWA ELIMU YA FEDHA NA NMB KATIKA KUMBUKIZI...

WAJASILIAMALI ZAIDI YA 1000 WAMEPATIWA ELIMU YA FEDHA NA NMB KATIKA KUMBUKIZI YA BIBI TITI RUFIJI

Wajasiliamali na Vijana zaidi ya 1000 wamepatiwa elimu ya fedha na kufungua akaunti za Banki ya NMB katika siku tatu za tamasha la kumbukizi ya Bibi Titi mwaka 2024 huko Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Hayo yamesemwa na Meneja Mahusiano Mwandamizi Huduma za Serikali wa Banki ya NMB Irene Masaki wakati akizungumza Waandishi wa Habari kuhusu tathimini ya Huduma zilizotolewa na Banki hiyo katika viwanja vya Ujamaa na maeneo mbalimbali ya vitongoji vya Mji wa Ikwiriri wilayani Rufiji.

Irene amesema Banki hiyo imetoa elimu kwa njia ya matangazo na hamasa kwa kutumia magari mitaani, masokoni na kwenye makusanyiko makubwa ya watu.

Amesema kundi linginge ni la watoa huduma wa Banki hiyo ambao wamekuwa wakisambaa mitaani na kwenye makusanyiko makubwa ya watu kuongea na wajasiliamali na mtu mmoja mmoja wakiwafungulia akaunti za Banki hiyo.

Irene amesema kati yao wajasiliamali Wanawake zaidi ya 400 walikutanishwa katika Ukumbi wa Chuo cha maendeleo ya jamii FDC na kupatiwa elimu mbalimbali kuhusu Huduma zinazotolewa na Banki hiyo ya NMB ili na wao wajiunge wanufaike na huduma hizo ikiwemo huduma ya mikopo.

Kundi jingine lililopata elimu ya fedha kuwa ni pamoja na madereva bodaboda ambao wamesisitizwa umuhimu wa kuweka akiba na aina za mikopo inayotolewa na Banki hiyo.

Amezitaja baadhi ya elimu iliyotolewa kuwa ni pamoja na elimu ya fedha, umuhimu wa kuweka akiba katika kila wanachopata, aina ya mikopo inayotolewa na Banki hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!