Home Kitaifa UVCCM TAIFA HAWANA HOFU MASHIRIKIANO YA KUIMARISHA UCHUMI WA BANDARI

UVCCM TAIFA HAWANA HOFU MASHIRIKIANO YA KUIMARISHA UCHUMI WA BANDARI

Na Magrethy Katengu

Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Serikali inachofanya sasa ni mashirikiano ya Uwekezaji Bandarini ili kwenda kusaidia kuimarisha miundombinu ya bandari na shughuli nyingine za lojistiki na Uchukuzi ili Taifa liwe kitovu cha uchumi Imara.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohamed Kawaida amesema kinachofanyika siyo kitu alichoamua mtu binafsi bali ni maelekezo ya Chama kupitia ilani yake ya uchafuzi mwaka 2020/2025 na ndiyo inayounganisha moja kwa moja na Serikali iliyopo madarakani hivyo kupitia ilani yake kupitia ibara 22(1) Chama kimeeleza kuondoka urasimu na dosari zinazosababisha ucheweshwaji wa utoaji mizigo Bandarini.

Hata hivyo amesema licha ya kusambaa mizozo mitandaoni kuhusu bandari katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 (a) na nukuu “kila mtu anao Uhuru wa kuwa na maoni ya kueleza fikra zake “hivyo tunaheshimu maoni ambayo yanatolewa na yanayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali kuhusu azimio hilo ambalo linaridhiwa na Bunge kwa mujibu ya Ibara 63-3(e)ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotaka Mkataba unaoingiwa na Serikali upitiw Bungeni kabla ya kutekeleza .

“Serikali ni kwelo Tanzania imeingia Mkataba wa mashirikiano na serikali ya Dubai kwa kuanzisha Ushirikiano wa kuboresha ,kuendesha na kuendeleza maeneo ya bandari nchini suala ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa serikali kufikia malengo ya kiuchumi na kijamii na majadiliano haya na maandalizi yanafanywa na Timu ya wataalamu wa Tanzania ambao Wana uzoefu mkubwa katika Masuala ya mikataba ya kinataifa na kabla ya kusainiwa ulizingatia taratibu zote za nchi yetu” amesema Kawaida

Hata hivyo amebainisha kuwa Ushirikiano pamoja na mambo mengine unajikita kwenye maboresho uendeshaji wa shughuli za bandari nchini kwa kuongeza tija na ufanisi kusimika mfumo ya kisasa ya TEHAMA na kuwajengea uwezo kupitia mafunzo Watanzania katika uendeshaji wa shughuli za bandari kuhusu changamoto za bandari mifumo ya TEHAMA ya bandari kisasa na inayosoma na mifumo mingine ikiwemo Mamlaka ya Mapato TRA hali inayosababisha kutokuwa na udhibiti wa kutosha katika kukusanya mapata ya nchi.

Aidha ifahamike kuwa jitihada zote na hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali ya Awamu ya sita katika kuvutia uwekeza nchini hususani kwenye maeneo ya bandari nchini zinalenga kumalizia changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshwaji wa meli mizigo na kukosekana kwa ufanisi katika bandari zetu ambako kumekuwa kukichangia katika sekta zingine .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!