Home Kitaifa TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TISHIO LA MGOMO WA WAFANYAKAZI MADEREVA

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TISHIO LA MGOMO WA WAFANYAKAZI MADEREVA

Serikali imetoa tamko kuhusu tishio la mgomo wa wafanyakazi madereva, taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Joyce Ndalichako kwa Waandishi wa Habari, tarehe 24 Julai, 2022.

Mhe,Ndalichako amesema mnamo tarehe 22 Julai, 2022 Serikali
ilitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu hatua zilizochukuliwa katika
kushughulikia Hoja na Malalamiko yaliyowasilishwa na Viongozi wa Vyama vya
Wafanyakazi Madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji nchini.

“Kufuatia
kutolewa kwa taarifa hiyo, wapo baadhi ya Madereva ambao wameipokea kwa
mtazamo tofauti. Kutokana na hali hiyo, wamekuwa wakipotosha taarifa hiyo na
kuchochea ama kuhamasisha Madereva wenzao kugoma” amesema Mhe.Waziri.

Aidha amesema uchochezi wa mgomo wao
umejikita katika viwango vya posho ambavyo Madereva, Wamiliki wa Vyombo vya
Usafiri na Serikeli waliafikiana katika vikao vya MAJADILIANO, akifafanua zaidi Mhe. Waziri amesema viwango walivyokubaliana ni viwango vya chini vya posho za safari (Minimum allowances) ambapo waajiri hawaruhusiwi kulipa chini ya viwango
hivyo. Kwa wale Waajiri ambao walikuwa wanalipa viwango ambavyo viko juu ya
viwango vya chini vya posho za safari vilivyowekwa, hawaruhusiwi kushusha viwango
hivyo kwani kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria, No.1

” Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya usafirishaji kwa uchumi
wa nchi, inasisitiza kuwa nafasi ya majadiliano bado ipo wazi na hivyo Wafanyakazi
Madereva ambao wana hoja na malalamiko zaidi ya yale yaliyofanyiwa kazi, wayawasilishe
rasmi katika mamlaka zinazohusika ili yaweze kupatiwa ufumbuzi”amesema.

Pia Mhe.Waziri amewasihi Wafanyakazi Madereva wapokee kwa mtazamo chanya
taarifa ya Serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa katika kushughulikia Hoja na Malalamiko
yaliyowasilishwa na Vyama vyao na Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji.

“Ninawasihi Wafanyakazi Madereva wote kuendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida,natoa rai kwa makundi yanayojihusisha kuchochea migomo ya Madereva kuacha mara moja, kwani kufanya hivyo ni kukiuka Sheria Serikali haitasita kuchukua hatua stahiki kwa wale wote watakaoendelea kuchochea migomo ya Madereva”alisema Mhe.Ndalichako.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!