Home Kitaifa MAFANIKIO YA TANZANIA KUFIKISHA UMEME VIJIJINI YAWAVUTIA REA ZAMBIA KUJA KUJIFUNZA

MAFANIKIO YA TANZANIA KUFIKISHA UMEME VIJIJINI YAWAVUTIA REA ZAMBIA KUJA KUJIFUNZA

Mafanikio makubwa ya Tanzania katika usambazaji wa umeme Vijijini yameifanya kuwa kivutio cha kujifunza kwa baadhi ya nchi Barani Afrika, baada ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupokea na kufanya kikao na Uongozi wa Mamlaka ya Umeme Vijijini (REA) kutoka nchini Zambia.

Akizungumza mara baada ya kikao cha pamoja kati ya Taasisi hizo kilichofanyika leo Jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa REA Tanzania, Mhandisi Hassan Saidy amesema kuwa ujio wa ugeni huo kutoka REA Zambia ni ishara ya kutambuliwa kwa mafanikio yaliyofikiwa nchini katika kupeleka huduma ya umeme kwa wananchi vijijini.

“Wageni wetu wamekuja kujifunza na kubadilishana ujuzi mara baada ya kuona mafanikio makubwa sana ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) yaliyofikia hasa ya kupeleka nishati ya umeme pamoja na nishati ya kupikia kwenye maeneo ya vijijini,” amesema Mhandisi Saidy.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa REA Zambia, Mhandisi Alex Mbumba ameipongeza REA Tanzania kwa mafanikio ya kufikisha umeme vijiji vyote vya Tanzania Bara hali inayokwenda kuchochea uchumi na kuboresha huduma za kijamii vijijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!