Home Kitaifa WAZIRI NDALICHAKO AHIMIZA USHIRIKI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI.

WAZIRI NDALICHAKO AHIMIZA USHIRIKI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako ametoa wito kwa wanaparokia wa Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni jijini, kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi itakayo fanyika tarehe 23 mwezi Agosti 2022.

Akiongea wakati wa Harambee ya kutegemeza Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni ambayo imeabatana na kilele cha Sikukuu ya Mavuno leo tarehe 24, Jijini Dar es Salaam, amesisitiza kuwa zoezi la sensa ni muhimu kwa Taifa katika kupanga mipango ya maendeleo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako akisistiza jambo wakati wa Harambee ya kutegemeza Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni tarehe 24, Jijini Dar es Salaam.
 

“Serikali yetu ikiwa na idadi kamili ya watu wa makundi mbalimbali ili kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinagawiwa kulingana na mahitaji, hivyo niwasihi watu wote tujiandae kuhesabiwa”

Aidha, katika hatua nyingine Mhe. Ndalichako amewapongeza wanaparokia hao hususani wanajumuiya ambao wamevuka malengo ya kukusanya michango kwa ajili ya kutegemeza Parokia yao, hivyo amewasihi waendelee kujiwekea hazina kwa Mwenyezimungu.

Wanaparokia wa Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni wakifuatilia Harambee ya kutegemeza Parokia ya hiyo  tarehe 24, Jijini Dar es Salaam.

“Kila mmoja wetu atoe kwa ajili ya Mwenyezimungu, ukitoa kwa ajili yake unakuwa umeiweka hazina yako katika mahala salama, tunapo toa tusiangalie thamani ya kitu bali thamani ya uwekezaji kwa Mwenyezimungu”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako akiendesha mnada wa kuuza Picha ya kuchora wakati wakati wa Harambee ya kutegemeza Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni tarehe 24, Jijini Dar es Salaam.
 

Kwa upande wake Baba Paroko wa Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni, Padri Gallen Mvungi amewasihi wanaparokia hao kuendelea kushkamana na kushirikiana katika kutoa michango ili waweze kufikia malengo ya makusanyo waliyoyaweka kwa mwaka huu.

Baba Paroko wa Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni, Padri Gallen Mvungi akiendesha mnada wa kuuza Kitabu wakati wa Harambee ya kutegemeza Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni tarehe 24, Jijini Dar es Salaam.

Shughuli ya Kutegemeza Parokia hiyo imefanyika siku ya kilele cha Sikuu ya Mavuno ikiwa na ujumbe kutoka Zab:50-54, Mtolee Mungu Dhabihu za kushukuru, Mtimizie aliye juu Nadhiri zako.

Wanaparokia wa Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni wakifuatilia Harambee ya kutegemeza Parokia ya hiyo  tarehe 24, Jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!