Home Biashara SERIKALI INATATUA CHANGAMOTO ZA VIWANDA VYA KATANI

SERIKALI INATATUA CHANGAMOTO ZA VIWANDA VYA KATANI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt .Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazovikabili viwanda vya kuchakata katani ili kuliendeleza zao hilo la kimkakati katika kukuza biashara, kuongeza ajira na kuongeza pato la taifa.

Waziri Kijaji amesema hayo alipokuwa akiongea na wafanyakazi wa Kiwanda cha 21st Century Holdings LTD kinachojihusisha na uchakataji wa kamba zinazotokana na mkonge kilichopo Chang’ombe jijini Dar es salaam, mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho leo Juni 17, 2022

Akiongea na wafanya kazi hao Dkt. Kijaji amesema katika kutatua changamoto hizo Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye mazao yote yanayotokana na zao Mkonge ikiwa ni lalamiko lao kubwa la wenye viwanda vinavyozalisha bidhaa za katani.

Pia Amesema Serikali inaendelea kushughulikia changamoto nyingine uli kuviwezesha viwanda hivyo kushiriki kikamilifu katika soko la ushindani ndani ya nchi kikanda na kimataifa

Aidha amewahakikishia wafanyakzi wa kiwanda hicho kuwa kiwanda hicho hakitafungwa kwa kuwa Serikali inashughulikia changamoto zinazokikabili kiwanda hicho pamoja na zinazowakabili wafanyakazi hao ikiwemo upatikanaji wa haki zao za msingi iwapo kiwanda hicho kitafungwa kwa kufuata sherua na taratibu zilizopo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!