Home Kitaifa MSHINDI WA TIGO CHEMSHA BONGO AKABIDHIWA MILIONI 10

MSHINDI WA TIGO CHEMSHA BONGO AKABIDHIWA MILIONI 10

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni namba moja nchini Tanzania kwa Utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo , Imekabidhi Hundi ya Milioni 10 kwa Mshindi wa Tigo Chemsha Bongo .

Michael V. Mang’ang’ara Mkazi wa Mbeya ndiye aliyeibuka mshindi wa Tigo chemsha bongo na kujishindia Shilingi Mil 10, alipatikana baada ya kujibu maswali rahisi kuhusu Muziki na sasa ameibuka mshindi wa Mil 10.

Akabidhiwa na meneja mauzo wa Tigo mkoa wa Mbeya, Bw. Ronald Richard pamoja na Nurdin Lugembe-mtaalamu huduma wa ziada Tigo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Hundi hiyo Mtaalam wa Huduma za ziada Tigo Bwn. Nurdin Lugembe amesema kuwa
” Imagine unaburudika na muziki na Bado @tigo_tanzania wanakuzawadia pesa , hiki ndicho kilichotokea kwa mshindi wetu wa Tigo Chemsha Bongo Bwn. Michael , nawewe Mteja wa Tigo unaweza kuibuka mshindi
Cha kufanya ni kujibu maswali mara kwa mara kuhusu Muziki ujiwekee nafasi ya kushinda Tuma neno muziki kwenda namba 15571

Naye kwa upande Bwn. Michael ambaye ndiye mshindi amesema kuwa sio mara yake ya kwanza kuwa mshindi , ameshawahi kuwa mshindi wa laki tano tano mara mbili na leo anajivunia sana kuibuka mshinda wa Donge nono la Milioni 10

” Nawasihi Watanzania wenzangu na wateja wa Tigo wasikate tamaa waendelee kucheza Tigo Chemsha Bongo wataibuka washindi kama mimi “. Alimalizia.

Naye Meneja Mauzo Mkoa wa Mbeya Bwn. Ronald Richard amempongeza mshindi na kuwasihi watanzania wacheze kwa wingi Tigo Chemsha Bongo na kutumia huduma nyingine mbalimbali za Tigo maana kutumia Tigo kunalipa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!