Home Kitaifa WIZARA YA MAMBO YA NJE NA CRDB WAWEKEANA SAINI UANZISHWAJI WA DAYASPOLA...

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA CRDB WAWEKEANA SAINI UANZISHWAJI WA DAYASPOLA DIGITAL APP

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na benki ya CRDB PLC wamefanya zoezi la utiajai saini hati ya makubaliano ya kutengeneza mfumo wa kidigitali wa kuhifadhi data za Wizara (Dayaspola Digital APP).

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Joseph Sokoine amesema mfumo huo wa kidigitali ni wapekee kugunduliwa ambao utasaidi Wizara kuratibu taarifa za Dayaspola wote walipo maeneo mbalimbali.

Pia Balozi Sokoine amesema utaratibu unaweza kuanza rasmi kwakuwa benki ya CRDB wametoa kiasi cha shilingi Milioni Mia moja na Wizara inaimani kuwa wataendelea kushirikiana pamoja kwenye mambo mengine kwajili ya maendeleo ya Taifa la Tanzania.

“Mfumo huo una fursa zaidi kutekeleza kwa vitendo, unaendana na mabadiliko ya Dunia na itasukuma gurudumu la maendeleo kwa ujumla”amesema Barozi Sokoine.

Sanjari na hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB PLC Abdulmajid Nsekela amesema benki yao inafursa ya kusikiliza wazo hilo wameona ni zuri sana itasaidia Nchi kutoka kwenye mifumo ya analojia kwenda digitali.

“Kwabkuanza mfumo huu kutakuwa na mafanikio makubwa utasaidia kutambua Dayaspola wote waliopo maeneo mbalimbali Duniani na shughuli zao wanazo fanya ili kuweza kupata msaada wa Nchi endapo watahitaji au wakipatwa na tatizo “amesema Nsekela.

Vilevile Mkurugenzi wa Dayaspola Balozi James Bwana amesema mfumo ameongezea kwa kusema mfumo huo utawezesha Dayaspola kujisajili na kupata huduma ya mtandao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!