Home Kitaifa RC MGUMBA ATEMBELEA KANISA WADIVENTISTI WASABATO TANGA.

RC MGUMBA ATEMBELEA KANISA WADIVENTISTI WASABATO TANGA.

Na Boniface Gideon, TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omar Mgumba Leo amefanya ziara ya kutembelea Kanisa la Waadventist Wasabato Kana Jijini Tanga kwaajili ya kujenga Mahusiano yakushirikiana katika kuwatumikia Wananchi,

Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa aliambatana na Mustahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahamani Shillow.

Akizungumza na viongozi wa Kanisa Hilo Mkuu huyo wa mkoa alisema lengo ni kujitambulisha kwa Viongozi wa Dini kwa kuwafuata katika Taasisi hizo na kufahamiana pamoja na kushirikiana kwa pamoja katika kuwatumikia Wananchi,
Nimekuja hapa katika Kanisa la Waadventisti Wasabato Kana nimekutana na Watumishi wa Kanisa Hilo lakini pia natembelea na Taasisi nyengine , Lengo ni moja tu lakuwatumikia Wananchi wetu, Viongozi wa Dini na Taasisi zao zinamchango mkubwa Sana kwenye Jamii yetu” Alisisitiza Mgumba

Mgumba aliongeza kuwa
nimeletwa na Rais Samia kuja kufanya kazi ili kuweza kuleta maendeleo na kutatua changamoto ambazo zipo katika jamii,na viongozi wa Dini pia wanawaongoza watu hivyo kuja hapa itaniwezesha kuweza kujua changamoto ambazo zipo katika jamii ” Alisisitiza Mgumba

Kwaupande wake Mchugaji Julius Mbwambo wa Kanisa hilo la Wadventista Wasabato Alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa ziara hiyo ambayo hawakuitegemea kuipata kutoka kwa viongozi wa Serikali,

Tunamshukuru Sana Mkuu wetu wa Mkoa wa Tanga kwakututembelea, sisi kwetu imetupa faraja Sana kwanza hatukutarajia kupata Ugeni kama huu kufika kanisani kwetu lakini, sisi kama Kanisa tupo Tayari kushirikiana nae lakini pia kushirikiana na Serikali katika kuwatumikia Wananchi mana wote ni Wananchi tofauti tu wakija kanisani wanaitwa Waumini ila wakitoka hapa kanisani wanaitwa Wananchi” Alisisitiza Mbwambo

Aidha Mchungaji Mbwambo aliwataka Waumini wa Kanisa Hilo pamoja na Wananchi kwaujumla kutoa Ushirikiano Wakati wa Sensa ,

Sote tunafahamu kuwa Nchi yetu ipo kwenye Zoezi la kuhesabu Watu na Makazi Sensa , niwaombe Waumini wetu na Wananchi kwa Ujumla tutoe Ushirikiano ili kufikia Malengo ya Taifa letu , Sensa ni jambo la Muhimu Sana katika Taifa lolote ulimwenguni hivyo tujitokeze kuhesabiwa ” Alisisitiza Mbwambo

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!