Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Agosti 23, 2022 amehesabiwa na kutoa majibu ya dodoso kuu la Sensa ya Watu na Makazi katika Makazi yake ya Kijiji cha Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi.
Akizungumza baada ya kuhesabiwa Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kuhesabiwa na kutoa taarifa kwa makarani wa Sensa ili taarifa hizo ziweze kutumika katika kupanga mipango ya maendeleo.
Aidha Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa zoezi la sensa litaiwezesha Tanzania kushiriki kwa pamoja mipango ya dunia ikiwemo mashirika mbalimbali ya kimataifa “Mashirika haya yakijua tupo wangapi yatakuwa na nafasi kubwa ya kujua namna ya kutusaidia”