Home Kitaifa KINANA AKOSHWA NA JITIHADA ZA SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUJIAJIRI NA KUAJIRIWA

KINANA AKOSHWA NA JITIHADA ZA SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUJIAJIRI NA KUAJIRIWA

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Abdulrhaman Kinana ametembelea Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kufurahishwa kwake na jitihada zinazofanywa na Serikali kuweka mazingira mazuri ya wananchi kushiriki shughuli za uchumi.

Lakini jambo kubwa zaidi ambalo limenifurahisha ni kila mshiriki alivyoweza kuonesha juhudi anazofanya katika kuchangia uchumi wa Taifa letu , maendeleo ya Taifa letu na kwa namna kujaribu kutatua tatizo la ajira kwa vijana lakini kukuza uchumi wa nchi.

Nimeona kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara kwa kutengeneza viwanda vidogo vidogo vitakavyowezesha wakulima mbalimbali kama vile wa sukari,alizeti na mazao mengine kuwa na viwanda vyao vidogo vidogo na kutengeneza bidhaa katika eneo dogo na kwa idadi ndogo ya watu

Amesema ameona namna ambavyo kumekuwa na bunifu mbalimbali kutoka kwa washiriki ambao utasaidia watu kujitegemea huku akieleza kwa mazingira na jitihada zinazofanyika kuna uwezekano wa mahitaji mengi kama sukari na mafuta na bidhaa nyingine zikawa zinapatikana hapa hapa nchini.

“Kwa hiyo nawapongeza Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa namna wanavyoweza kuwasaidia vijana wetu kujiari na kuajiriwa na mara nyingi tunataka vijana wajiajiri lakini tusipotengeza fursa za watu kujiajiri, na mazingira ya watu kujiajiri kauli itabaki kuwa kauli bila utekelezaji.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!