
Na Magrethy Katengu–Mzawa Media
Chama cha National League for Demokracy (NLD) Kimemuidhinisha Doyo Hassan Doyo kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama.hicho katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 huku Mfaume Khamisi Hassani akiidhinishwa kiwania Urais wa Zanzibari
Akizungumza Aprili 10,2025 Jijini Dar es salaam baada ya Uchaguzi huo amesema Chama hiko wanalipenda Taifa la Tanzania na hawapo tayari kujihusisha na chama chochote kutoshiriki Uchaguzi hivyo watashiriki zoezi hilo mpaka mwisho huku wakihakikisha wanalinda tunu ya Amani iliyopo
“Chama cha NLD tutaweka wagombea Nchi nzima hatuko tayari kususia Uchaguzi wala kuleta sababu zisizo kuwa na mashiko tuna Imani Sera zetu zitawafikia watanzania watatuchagua“

Hata hivyo ameshukuru Chama chake kumuamini kuipeperusha kumpa dhamana ya kuwania Urais hivyo anaaihidi Watanzania wakimchagua atapambana na Mafisadi wala rushwa wote kwa kuweka adhabu ya viboko 24 kwa yeyeyote atakayebainika katika Serikali yake
Naye Mgombea Urais Zanzibari Mfaume Khamisi Hassani ameshukuru kwa chama hiko kumuamini kwenda kupeperusha bendera ya NLD atahakikisha Wazanzibari wakimpatia Kura Serikali itakayoundwa itashughulika kero za wananchi zote zilizokuwa zikiwakabili

Awali Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza ambaye lihudhuria kushuhudia Uchaguzi huo wa NLD amesisitiza kuwa chama chochote kilichosajiliwa kikatiba kinatakiwa kushiriki Uchaguzi hivyo amefurahishwa na mwenendo wa chama hiko