Home Kitaifa DC SAME APONGEZA JITIHADA ZA MASHIRIKA YASIYOKUWA YA KISERIKALI KWA MCHANGO WAKE...

DC SAME APONGEZA JITIHADA ZA MASHIRIKA YASIYOKUWA YA KISERIKALI KWA MCHANGO WAKE KWENYE JAMII WILAYANI SAME.

Na Dickson Mnzava,

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ameyapongeza mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa mchango wake mkubwa Katika kuihudumia jamii.

DC Mgeni ameyasema hayo kwenye jukwaa la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro ambapo amesema mchango wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi ni mkubwa na wao kama serikali wataendelea kuthamini kazi nzuri za mashirika hayo.

Amesema miradi ya maendeleo kwa wananchi haitegemei serikali pekee bali mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yana mchango mkubwa Katika kusaidiana na serikali kuwafikia wananchi kwa nyanja mbalimbali za maendeleo.


“Kweli kipekee niwashukuru sana mashirika yasiyokuwa ya kiserikali mmekuwa mkifanya mambo mengi makubwa kwenye jamii zetu na matunda yanaonekana lakini mmekuwa pia mkiipunguzia serikali mzigo wa kuwahudumia wananchi wake niwaombe endeleeni kufanya kazi zenu kwakuzingatia taratibu na sheria za Nchi na endeleeni kufanya kazi kwa kuzingatia maadili mema kwenye jamii na mimi kama kiongozi wa Wilaya nipo tayari kuwapa ushirikiano wakutosha katika kazi zenu lakini niwaombe kila baada ya miezi 3 kila mmoja atoe taarifa ya kazi zake anazozifanya kwa Mkuu wa Wilaya”
“Alisema DC Same Kasilda Mgeni”.

Akizungumza katika jukwaa hilo kaim Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro ambaye pia ni msajili msaidizi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wilayani Same Charles Anatol amewaasa viongozi wa mashirika hayo kufuata taratibu na sheria za Nchi katika utendaji wao wa kazi na kuzingatia maadili mema ya watanzania sambamba na miradi yao iweze kuigusa jamii moja kwa moja.

Adam Henry Mwashambo mjumbe wa baraza la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Mkoani Kilimanjaro amewasihi viongozi wa mashirika hayo wilayani Same kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa mashirika binafsi wilayani humo.

Henry amesema katika jukwaa hilo wamekutana zaidi ya mashirika 20 lakini kwaujumla yapo mashirika yasiyokuwa ya kiserikali 39 ndani ya Wilaya hiyo.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!