Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii uliofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha leo February 10, 2026.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ukumbi wa AICC Arusha kwa lengo la kufunga Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii uliofanyika leo tarehe 10 February, 2026.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano Bi. Mary Maganga (Kushoto) baada ya Waziri huyo kuwasili katika ukumbi wa AICC Arusha kwa lengo la kufunga Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii uliofanyika leo tarehe 10 February, 2026
Na. Antonia Mbwambo,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Arusha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete amesema Serikaili ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuimarisha sekta ya kinga ya jamii ili kuleta manufaa kwa umma.
“Rais anatamani na amedhamiria kwa dhati kuongeza wigo wa wananchi wanaopata huduma za kinga ya jamii hasa wale waliojiajiri katika sekta isiyorasmi, hivyo ninaimani kuanza kutumika kwa Sera Mpya ya Kinga ya Jamii ya mwaka 2023 itawanufaisha wananchi” alisema Mhe. Kikwete.
Ameyasema hayo Februari 10, 2026 wakati akizungumza na kufunga Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii uliofanyika katika Ukumbi wa AICC- Jijini Arusha.
Ameongeza kuwa, dhimira hii ya Rais imesababisha kutungwa kwa Sera ya Kinga ya Jamii ya mwaka 2023 na imezinduliwa rasmi tarehe 9 Fesbruari 2026. Sera hiyo inalenga kuhimiza wananchi wote wenye uwezo wa kuzalisha kipato wananjiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii. Lengo la mwelekezo ili kila mtanzania anufaike na huduma za Kinga ya Jamii kwa uchangiaji zinazotolewa na NHIF, PSSSF na NSSF.
Aidha, alifafanua kuwa, Kinga ya Jamii ni uwezeshaji wananchi kupitia michango inayotolewa kwa njia mbili ambazo ni watumishi wa umma na wa sekta binafsi wanaopata mshahara kuchanga wenyewe na wananchi wasiojiweza mathalani wazee, akina mama na watoto kusaidiwa kwa kuchangiwa na Serikali kupitia mifuko na programu mbalimbali.
“Sisi Tanzania ni moja kati ya nchi 17 Barani Afrika ambazo zimefanikiwa kutekeleza eneo la kinga ya jamii kwa kuwezesha wananchi kupitia michango inayotolewa na watumishi wa umma au watumishi walio katika sekta binafsi na wale wasio na uwezo wanachangiwa na Serikali” alisema Mhe. Kikwete
Mhe. Kikwete alisisitiza kuwa, Tanzania ina kila sababu ya kujivunia jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao unawasaidia wananchi kuinuka kiuchumi, hvyo kuifanya Tanzania moja ya nchi barani afrika zinazowafikia wananchi wengi katika sekta isiyorasmi.
Vile vile, aliwashukuru na kuipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano kwa kuandaa mkutano wa wadau wa Sekta yak inga ya jamii na kuimarisha mazingira wezeshi ya utekelezaji wa sekta ya Kinga ya Jamii ambayo itainua maisha ya watanzania walio wengi.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii uliofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha leo February 10, 2026.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano Bi. Mary Maganga (Kulia), baada ya Waziri huyo kuwasili katika ukumbi wa AICC Arusha kwa lengo la kufunga Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii.
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii, wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo akitoa hotuba ya Kufunga Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha leo February 10, 2026.
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii, wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo akitoa hotuba ya Kufunga Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha leo February 10, 2026.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii uliofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha leo February 10, 2026.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na bodi ya wadhamini wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii uliofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha leo February 10, 2026.








