Home Kitaifa WAKAZI WA DIGUZI MORO WAPATA MWAROBAINI WA KUONDOKANA NA KERO YA MAJI

WAKAZI WA DIGUZI MORO WAPATA MWAROBAINI WA KUONDOKANA NA KERO YA MAJI

Zaidi ya wakazi 2000 wa Kijiji Cha Diguzi Kata ya Ngerengere Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wamenufaika na Mradi wa Maji Diguzi ambao unaenda kutatua changamoto ya ukosefu wa maji ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wakazi hao.

Mradi huo uliogharimu zaidi ya Milioni 300 unaenda kuwa mwarobaini kwa wakazi wa eneo hilo baada ya kuwekwa jiwe la msingi na mwenge wa Uhuru ambao umeanza mbio zake katika Halmashauri hiyo

Akizindua mradi huo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ali Ussi amesema Serikali ya awamu ya sita imemaliza changamoto ya maji katika kijiji hicho hivyo amewasihi kuutunza mradi huo

Huku baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wameipongeza Serikali kwani walikuwa wakitembea umbali wa muda mrefu kufuata huduma ya maji mto Ngerengere

Mwenge wa uhuru 2025 umepokelewa leo Aprili 11, 2025 Mkoani Morogoro na Mkuu wa Mkoa huo Adam Malima kutoka Mkoa wa Pwani na unatarajia kupitia miradi 70 ya maendeleo yenye thamani ya Tsh. Bil. 18.5 ambayo inapatikana Halmashauri zote 9 za Mkoa wa Morogoro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!