Home Biashara TIGO NA NOKIA WALETA SIMU MPYA SOKONI KWA BEI NAFUU

TIGO NA NOKIA WALETA SIMU MPYA SOKONI KWA BEI NAFUU

 Leo tarehe 8 Julai 2022 , Kampuni namba moja ya huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo pamoja na Kampuni ya Simu za mkononi ya NOKIA  wametambulisha simu mpya za NOKIA C1 na NOKIA C10 zenye muonekano wa kijanja, uwezo mkubwa na bei nafuu.

Akizungumza wakati wa kutambulisha simu hiyo Meneja wa vifaa vya intaneti  kutoka kampuni ya Tigo Bwana Edwin Mgoa amesema simu hizo ziapatikana kwenye maduka ya Tigo na NOKIA Nchi Nzima huku ikiwa na Ofa ya Intaneti ya GB 96  kwa mwaka BURE, Ikiwa ni dhamira ya Kampuni ya Tigo kuleta simu hizi nzuri na za kisasa Ili kuhakikisha wateja wake wanakwenda kwenye mawasiliano ya Kidigital na kutimiza dhamira ya serikali ya kuhakikisha kwamba kufikia mnamo 2025 asilimia 80 ya vifaa vya mawasiliano vinakidhi TEHAMA kwa mfumo wa Kiserikali.

Naye kwa upande wake , Mwakilishi kutoka NOKIA  Bi. Winfrida Marila amesema kuwa ujio wa NOKIA C1 na C10 sokoni ni mwendelezo wa C series ambapo Nokia kwa kuwajali wateja wake inazidi kuleta kilicho bora sokoni 

” Nokia C1 na Nokia C 10 ni simu bora na za kisasa  zenye sifa ambapo  C 10 Ina Ram 2 na Gb 32 pia Ina warranti ya mwaka mzima, Ina kioo kikubwa kwa wanaopenda kuangalia movies pia Ina security update ya miaka mitatu hii ina maana kuwa mteja atakaponunua mfano Nokia C 10 ataweza ku update bila kulazimika kununua toleo jipya, 

Na kwa upande wa Nokia C 1 second edition Ina Ram 1 kwa Gb 16 ni affordable kwa watu wote , kumbuka simu zote hizi zinapatikana katika maduka ya Tigo na NOKIA nchi nzima na kwa bei Nafuu , Karibuni mnunue simu na kujipatia zawadi kedekede kutoka kwetu NOKIA pamoja na Washirika wetu Tigo Tanzania ” alimalizia Bi. Winfrida

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!