Home Kitaifa TBS NA WATAALAM WA VIWANGO AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA KUJADILI NA KUWEKA MFUMO...

TBS NA WATAALAM WA VIWANGO AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA KUJADILI NA KUWEKA MFUMO MAALUM WA KUSIMAMIA USALAMA WA CHAKULA

Na Mwandishi Wetu

Shirika la Viwango Tanzania ( TBS )  limeandaa Mkutano wa Siku nne na wataalam ( Trainers ) wa kila nchi hasa nchi za Afrika Mashariki ili waweze kwenda kwao na kusambaza elimu juu ya Umuhimu wa Kuwepo kwa mfumo Maalum wa kusimamia Ubora wa Chakula ( Food Safety System ) , Mkutano unaofahamika kama Training on ISO 22000 Food Safety Management TOT Program.

Akizungumza Leo Machi 04, 2024 wakati akifungua Mkutano huo wa Siku Nne utakaofanyika Jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS Prof. Othman Chande amesema

Mkutano huu ni wa maana sana kwasababu utazifanya nchi zote hasa za Afrika Mashariki kuwa na Kiwango Kimoja ili kuiendeleza biashara na kuhakikisha Chakula chetu kiko salama na kuweka Mfumo Maalum wa kusimamia Ubora wa Chakula. 

Naye kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Athuman Ngenya amesema

Mkutano huu ni Mpango Maalum ambao umeandaliwa na Shirika la Kimataifa linalohusu Viwango ( ISO ) katika kusaidia nchi zenye uwezo mdogo hasa za Afrika Mashariki katika kuzipa uwezo wa kuweza kujua na kuvichukua viwango vya Kimataifa vinavyohusu Usalama wa Chakula , suala litakalopelekea Bidhaa zetu kuingia moja kwa moja katika Soko la Kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!