Home Biashara SMZ KUSAINI MAKUBALIANO NA WAWEKEZAJI KISIWA CHA MNEMBA-Mhe. SORAGA

SMZ KUSAINI MAKUBALIANO NA WAWEKEZAJI KISIWA CHA MNEMBA-Mhe. SORAGA

Ameyasema hayo Waziri wa Nchi – Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga wakati akitoa taarifa fupi ya mwenendo wa uwekezaji katika kisiwa hicho, katika kikao cha kumi (10) mkutano wa nane (8) wa Baraza la Kumi na wawakilishi linanaendelea huku katika ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Amesema mnamo mwezi wa oktoba mwaka huo Serikali kupitia idara ya uhifadhi wa mazingira baharini itasaini mapitio mapya ya mkataba wa maelewani (Memorandum of Understanding) na wawekezaji hao kwa ajili ya kulinda uhifadhi wa mazingira pamoja na kuingiza kiasi kikubwa cha pesa kupitia utalii wa hadhi ya juu unaokusudiwa kufanyika Zanzibar.

Amesema ili kuyalinda mazingira ya kisiwa hicho Serikali imeweka ushuru maalum wa uhifadhi wa mazingira kwa watalii watakaokitumia kisiwa hicho na inatarajiwa kukusanya kiasi cha dola za kimarekani 75 sawa na shilingi 174,932.31 kwa kila mgeni mmoja kwa siku ambayo ni sawa na dola laki tatu na arobaini (792,709,967,121 TZS) kwa mwaka ambapo sehemu ya fedha hizo itarud kwa jamii moja kwa moja kiasi cha dola laki moja na elfu mbili (2,335,863,042) kila mwaka.

“Kuna utaratibu ambao unatakiwa uwekwe kwa wageni wa kila siku wanaokwenda kwenye kisiwa ambao wameekewa tozo maalumu amabyo watakiwa walipe dola $25 kwa siku kwa kila mgeni.” Alisema Soraga.

Aidha Waziri Soraga amesema awali wawekezaji hao walikuwa wanalipa kiasi ya dola elfu tano tu kwa ajili ya kilemba cha Matumizi ya Ardhi (Land Lease Agreement) kwa mwaka lakini sasa makubaliano hayo mapya watalazimika kulipa kilemba hicho dola za kimarekani milioni tatu na laki tano (8,162,587,280 TZS) ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.

Sambamba na hayo pia wawekezaji hao wametenga jumla ya fedha dola laki sita (1,399,119,510 TZS) kwa ajili ya kubuni ukarabati wa kisiwa kicha kwa ajili ya kuzuia mmon’gonyoko wa ardhi pamoja na kukubali kutumia nishati ya umeme wa jua (Solar Power) ili kulinda haiba na uwepo wa kisiwa hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!