Home Kitaifa WAKAZI 3,500 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI KALAELA WILAYA YA KALAMBO

WAKAZI 3,500 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI KALAELA WILAYA YA KALAMBO

Na. OMM Rukwa
Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingia Vijijini (RUWASA) mkoa wa Rukwa imefanikisha upatikanaji wa majisafi na salama karibu na na wananchi kufuatia kukamilika kwa mradi maji wa kijiji cha Kalaela wilaya ya Kalambo utakaohudumia wakazi 3,588.

Akizungumza kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi leo (20.09.2022) Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma aliwapongeza RUWASA kwa kujenga mradi huo kwa ubora na kuwataka wahakikishe miundombinu iliyojengwa inakuwa imara na kuepusha maji kuvuja.

“tone la maji ni dhahabu hivyo watalaam pamoja na mkandarasi fanyeni jitihada ili eneo lote la mradi pia wananchi sasa wekeni huduma ya maji katika nyumba zenu” alisema Geraruma.

Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa RUWASA wilaya ya Kalambo Mhandisi Patrick Ndimbo alisema jumla ya shikingi Milioni 152.5 kati ya shilingi Milioni 436.5 zimetumika kujenga mradi mradi unaotekelezwa kupitia fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Mhandisi Ndimbo alieleza kuwa tayari mradi uulianza Februari mwaka huu na umefikia asilimia 90 na huduma ya maji imeanza kupatikana kwa wananchi wa kijiji cha Kalaela na utakamilika mwezi Octoba 2022.

Alitaja kazi zilizokamilika kuwa ni ujenzi wa bomba kuu umbali wa mita 600, ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lita 150,000, ujenzi wa bomb la kusambazia maji umbali wa mita 3,400 na ujenzi wa vituo nane vya kuchotea maji.

Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa ujenzi vyumba vinne vya madarasa katika shule ya sekondari Mwazye uliogharimu shilingi Milioni Themanini( 80,000,000).

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Tano Mwera alisema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa na kupitia miradi mitano kwa kuweka mawe ya msingi, kuzindua na kukagua ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni Moja na Milioni Themanini na Sita (1,086,800,000.0)

Kesho Jumatano, Mwenge wa Uhuru utaendelea na mbio zake katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbwanga.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!