Home Kitaifa SHAMRASHAMRA NDEREMO NA VIFIJO ZIFF ZANZIBAR JUNI 18 FILAMU GANI BORA ITAIBUKA...

SHAMRASHAMRA NDEREMO NA VIFIJO ZIFF ZANZIBAR JUNI 18 FILAMU GANI BORA ITAIBUKA KIDEDEA DUNIANI?

Ikiwa imesalia Masaa machache kuelelea katika Tamasha la ZIFF Zanzibari huku Wasanii waigizaji kutoka Nchi mbalimbali wanaotarajiwa kuhudhuria wakitafakari nini kitatokea mwisho wa Tamasha Nchi gani na ni Filamu gani itatamba siku hiyo

Akizungumza Dar es salaam Mratibu wa Tamasha la kimataifa la filamu Zanzibar(ZIFF) Prof Martini Muhando amesema Tanzania Filamu ya Vuta nikuvute ndiyo itakayozindua Tamasha hilo kwa kuanza kuonyeshwa huku usiku huo wa juni 18 zaidi ya watu 15 wageni ambao na Wamarekani weusi waliohamia Marekani watasafiri na Jahazi kutoka Bagamoyo kuelekea Zanzibari kufanya hivyo ni kusherekea na kutambua mchango wa watu Weusi katika Maendeleo ya Dunia ambapo siku hiyo iliamriwa na Umoja wa Mataifa ifanyike kila mwaka

“Wageni hao wametambua kuwa Afrika ni nyumbani kwao sisi tutawapokea kama watu huru ambapo mwaka 2021 Wamerekani waliwatambua Waafrika katika Maendeleo ya Dunia na kuitenga siku juni 18 ifanyika kila mwaka “alisema Profesa Muhando

Amesema Nchi zote zitashiriki kuonyesha Filamu zao na maonyesho ya kazi wanazozifanya na midahalo ikiendelea hadi pale majaji watakapomua ni Filamu gani itakayotamba kidunia

“Tutakuwa na Filamu 101 Filamu hizo zitatoka katika Nchi zote 33 zitakazoshiriki na litakuwa Tamasha la kipekee huku Nchi ya Irani Filamu zake 15 zitaonyeshwa

Profesa Muhando amesema Mwaka huu wanaanzisha jukwaa la kudumu ya ZIFF kwenye YouTube kwa filamu zilizopata kuoneshwa katika tamasha hilo yaani ZIFF@25 Retrospective. Mrejeo huo utajumuisha filamu ambazo zimeshinda au kuvutia katika ZIFF hivyo tumekusudia jukwaa letu la Youtube liwe kituo cha kuangalia nmajadiliano ya ambapo watengenezaji filamu wataweza kufikia hadhira muhimu na kufanya mazungumzo nao.

“Tunazungumzia fahari waliyonayo Watanzania kwa ujumla katika ZIFF, kwa kuwa miongoni mwa matamasha matatu bora ya filamu barani. ZIFF sio tu imedumu pale ambapo wengine wameshindwa bali pia imejitengenezea misingi imara wa kuendelea. Udhaifu wowote ambao ZIFF inaweza kuonyesha, tutabaki kujivunia hivyo, ndio maana tunasema Lake Mtu Halimtapishi!”alisema Prof Muhando

Naye Balozi wa Ulaya Nchi Tanzania Manfredo Faut amesema Utamaduni na Sanaa ni kitu cha muhimu kinatangaza Taifa na kinatengeneza fursa mbalimbali za ajira kiuchumi hivyo vijana wasibweteke wajitokeze kukuza vipaji vya walivyo navyo.

Pia Balozi wa Ufaransa Nabil Hjloui ameeleza kuwa Umoja wa Ulaya uko tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha wanazalisha Filamu bora kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ili waendane na soko la Kimataifa.

Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani Nchini Regina Hess amesema Tanzania na Ujerumani wana ushirikiano wa muda mrefu na kuna baadhi ya vitu vya kihistoria vipo Tanzania na baadhi ya wananchi wao huja kutembelea kama kufanya Utalii hivyo Tamasha hilo wanaopenda liwe endelevu kuwasaidia vijana kupata ajira.

Aidha watu wote wadau wanakaribishwa kushiriki katika tamasha na kutoa ushirikiano Kwa namna yeyote hivyo linalotarajiwa kuzinduliwa June 18 Mwaka huu Zanzibari na kuhudhuria na Mataifa 33 ikiwemo Irani, Afrika kusini, Kenya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!