Home Kitaifa DENI LA TAIFA TRILIONI 69.44

DENI LA TAIFA TRILIONI 69.44

Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania Dr. Mwigulu Nchemba leo Bungeni Dodoma kwenye hotuba yake akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 na mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2022/23 amesema hadi April 2022 deni la Taifa lilikua ni Trilioni 69.44.

“Hadi Aprili 2022 deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni 69.44 ikilinganishwa na shilingi trilioni 60.72 kipindi kama hicho mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 14.4 ambapo kati ya kiasi hicho deni la nje lilikuwa shilingi trilioni 47.07 na deni la ndani lilikuwa shilingi trilioni 22.37″

“Ongezeko la deni la Serikali lilitokana na kupokelewa kwa mikopo mipya kutoka vyanzo vyenye masharti nafuu na ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo, aidha ongezeko la deni lilitokana na kutolewa kwa hatifungani maalumu yenye thamani ya shilingi trilioni 2.18 kwa ajili ya deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) lililotokana na michango ya Watumishi wa kabla ya mwaka 1999”

“Taarifa ya tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Novemba 2021 inaonesha kuwa deni la Serikali bado ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika kimataifa”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!