Home Kimataifa SERIKALI YA TANZANIA YAKABIDHI MISAADA YA KIBINADAMU KWA SERIKALI YA MALAWI

SERIKALI YA TANZANIA YAKABIDHI MISAADA YA KIBINADAMU KWA SERIKALI YA MALAWI

NA: mwandishi wetu

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mhe. Humphrey Polepole ameshiriki katIka zoezi la kukabidhi misaada ya Kibinadamu kutoka Tanzania kwa Serikali ya Malawi ili kusaidia wahanga wa Kimbunga Freddy.

Balozi amekabidhi misaada hiyo ya kibinadamu inayojumuisha Mablanket, Mahema, Unga wa Mahindi kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi Mhe. Nancy Tembo katika Mji wa Blantrey Nchini Malawi mapema leo 25/03/2023.

Balozi Polepole alibainisha kuwa wa watanzania, na watu wa Malawi ni jamii moja, na Nia ni kuendekeza umoja uliojengwa na waasisi wa Nchi zetu.

” Msaada huu wa kibinadamu utasaidia, katika jitihada za kurejesha matumaini na ustawi kwa ndugu zetu Wananchi wa Malawi”, Alisisitiza Balozi Polepole.

Aliongeza kusema kuwa ana imani na wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania walioenda Nchini Malawi watashirikiana na wenzao Wanajeshi wa Malawi, kuhakikisha kwamba misaada iliyotolewa inawafikia Wahanga wa Kimbunga Freddy.

Aidha, Tanzania imetoa madawa ya binadamu, ambayo yataweza kusaidia kwenye maeneo ambayo vituo vya afya vimeathirika. Hizi zote ni jitihada za kusaidia Nchi ya Malawi katika kurejesha huduma za afya.

Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Msaada aliotoa kwa Nchi ya Malawi, kwa uwezeshaji wa fedha na wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Wahandisi wa Medani) ambao watasaidia katika kurejesha hali ya miundo mbinu Nchini Malawi,” alisema Balozi.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje wa Nchi ya Malawi Mhe. Nancy Tembo amesema ameshukuru Nchi ya Tanzania kwa Msaada wa kibinadamu iliowapatia, ambao umefika katika wakati muafaka.

“Msaada huu ni muhimu kwetu kwa sababu tunao Wanachi wengi ambao makazi yao yameharibika, na tunahitaji msaada wa kila mtu ili kuhakikisha wahanga wa Kimbunga Freddy wanapatiwa huduma za msingi kwa wakati,” alisema Waziri Nancy

Aliongeza kusema Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wamekuja kutusaidia na wataungana na askari wetu wa Nchini Malawi katika kurudisha miundo mbinu iliyoharibika katika hali ya kawaida.

Nachukua fursa hii kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutusaidia katika wakati ambao tunahitaji msaada sana, janga hili ambalo limeathiri Nchi ya Malawi, limegharimu maisha ya watu, na limeharibu miundo mbinu” alisema Waziri Nancy.

Naye Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulika na Operesheni pamoja na Uratibu wa shughuli za Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu Luteni Kanali Selestine Masalamado ametoa pole kwa wananchi wa Malawi kwa Maafa ya Kimbunga Freddy.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!