Home Kitaifa SERIKALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM YAANDAA MKAKATI KUWASAIDIA WATOTO WANAOISHI...

SERIKALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM YAANDAA MKAKATI KUWASAIDIA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

Na Magreth Mbinga

Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam inapanga mipango ya kusaidia watoto wa mitaani kuweka utaratibu wa kuwatoa mahali hatarishi na kuwaweka mahali salama kwa kujenga kituo maalumu ambacho kitaweza kutambua vipaji na fani sa watoto hao na kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Amos Makala katika warsha iliyoandaliwa maalumu kwaajili ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na kuwasilisha tathmini ya Sensa ya Mkoa wa Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee mkoani humo.

“Tunawatoa mtaani tunawapeleka mahali wanakaa wanaangaliwa vipaji vyao lengo ni kuwabadilisha kimaisha kimkakati watu ambao wamekata tamaa inabidi tuwasaidie kuwabadilisha kifikra wakiwa sehemu salama” amesema Mh Makala.

Pia Mh Makala amesema kituo hiko pia kitawasaidia watoto hao kupata mahitaji yao kwa urahisi kuliko wakiwa huko mtaani na maana ya kuwaweka hapo usalama wao pia utakuwepo pomoja na kuepushwa kutumika vibaya hasa katika matukio yanayotokea ya uhalifu.

“Maafisa Ustawi wa jamii mufanye kazi kwa karibu na hivyo vituo sio wakati wa majaribio tu kwani nyinyi ndio walezi ,muwaelekeze muwe wepesi hata kwenda magerezani kuangalia hawa watoto waliopo had ko” amesema Mh Makala.

Aidha Mh Makala amewataka wazazi na walezi kudumisha malezi maana watoto wa mtaani hawajapenda kuwa hivyo kwahiyo mzazi one mtoto wa mwenzake kama wake mtoto kufika katika mazingira magumu mzazi anachangia maana kuna watoto wengine wapo mtaani na wazazi wao wapo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!