Home Kitaifa MWALIMU NYERERE AKUMBUKWA KAMA MWANA DIPLOMASIA NAMBA MOJA NCHINI

MWALIMU NYERERE AKUMBUKWA KAMA MWANA DIPLOMASIA NAMBA MOJA NCHINI

Na Magreth Mbinga

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni mtu wa kujifunza na kusikiliza hata kama ukiwa mdogo atakupa utulivu wa kuweza kujieleza iwe ndani ya baraza au nyumbani kwake alikuwa mtu wa imani sana na diplomasia alijali muda.

Hayo yamezungumzwa na Spika wa Bunge Mstaafu Mh Anna Makinda katika kongamano la mchango wa Hayat Mwalimu Julius Nyerere katika kujenga na kuendeleza uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia Nchini kuelekea kumbukizi ya kifo chake Oktoba 14 lililofanyika jijini Dar es Salaam.

“Nidhamu ya kutunza muda alikuwa nayo asilimia mia moja hasara ya kitu ni kukosa kutunza muda wakati wa Mwalimu hata katika Baraza alitaka kwenda na muda kama ukichelewa kuingia ndani akifunga mlango huwezi kuingia tena hata kama tulikuwa na wasilisho la muhimu.

Pia Mwenyekiti wa Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam Balozi Ramadhani Mwinyi amesema anamkumbuka Mwalimu Nyerere kama mwana Diplomasia namba moja Nchini Tanzania yeye ndiye alianzisha Diplomasia kwa maana ya mahusiano ya Mataifa na yeye ndiye Rais wetu wa kwanza aliyetukomboa katika ukoloni.

” Aliweza kuunganisha Nchi zetu mbili kwa maana ya Tanganyika na Zanzibar na kuweza kuzaliwa Tanzania kwa maana hiyo hiyo no mwana Diplomasia namba moja na ameshiriki kukomboa Nchi nyingi za Afrika hakuwa tayari kuona Tanzania pekeyake inakuwa guru”amesema Balozi Mwinyi

Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Felix Wandwe amesema leo wameadhimisha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ukiwa in miaka 23 tangu kifo chake wao kama Chuo wanahusika sana na Hayat Mwalimu Nyerere wameanda kongamano la kwanza la Diplomasia la kukumbuka mchango wa Mwalimu katika Mahusiano ya Kimataifa.

“Mchango wa Mwalimu Nyerere ni mkubwa sana katika mahusiano ya Diplomasia mtakumbuka wote kwamba alikuwa muasisi wa sera ya mambo ya nje ambayo tunaendelea kuitumia mpaka sasa ambapo tinaibadilisha mara kwa mara ” amesema Wandwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!