Home Kitaifa RIDHIWAN KIKWETE APOKEA MSAADA WA VITANDA VYA WAGONJWA NA DARUBINI

RIDHIWAN KIKWETE APOKEA MSAADA WA VITANDA VYA WAGONJWA NA DARUBINI

Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Ridhiwan Kikwete amepokea Vitanda vya Wagonjwa kutoka Shirika la Lion Club kwa ajili ya uchunguzi, sambamba na Darubini ya kuchunguzia magonjwa mbalimbali.

Shirika hilo limetoa msaada huo kwa nia ya kusaidia huduma ya Afya katika jimbo hilo hususani Zahanati ya Ruvu Darajani ambapo amelishukuru shirika hilo huku akiwapongeza kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa vitendo katika kuhakikisha huduma za Afya zinazidi kuimarika.

Mhe. Ridhiwan katika jimbo lake amekuwa akisaidia wananchi wake kwa vitendo katika shughuli mbalimbali za kijamii sambamba na kuwatatulia changamoto wananchi wa jimbo hilo.

Mpango wa Serikali ni kuhakikisha suala la afya kwa wananchi linakuwa kipaumbele zaidi ambapo Mbunge huyo amekuwa mbele kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi kwa vitendo ukiwemo ujenzi wa vituo vya afya .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!