Home Kitaifa RC MTANDA ATAKA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA KLINIKI YA UTATUZI WA MIGOGORO...

RC MTANDA ATAKA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA KLINIKI YA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI

-ATUMIA SAA 7 KUWASIKILIZA WANANCHI

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Said Mohamed Mtanda amezindua klinick ya kusikiliza migogoro ya ardhi na kutaka kupokea taarifa ya utekelezaji wake.

Kauli hiyo ameitoa kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo ulipofanyika uzinduzi huo na kutumia saa 7 kuwasikiliza wananchi wenye kero na migogoro mbalimbali ya ardhi.

Amesema mkoa wa Mara hauna eneo la kutosha la ardhi kwani ni asilimia 27.8 wanalolitumia wananchi na mifugo na kutaka matumizi bora ya ardhi.

Amesema lengo la kuanzisha kliniki ya migogoro ya ardhi iliyozinduliwa ni kuwasikiliza wananchi na kupata utatuzi wake.

Mtanda amesema mara baada ya kliniki hiyo kupita anahitaji kupata taarifa ili kujua migogoro iliyopokelewa na kupatiwa ufumbuzi.

Mkuu huyo wa mkoa kliniki hiyo imewatoa watumishi wa ardhi ofisini na kuwafuata wananchi kwenye maeneo yao ili kuweza kuwasikiliza kero zao.

“Leo tumefanya uzinduzi wa kliniki hii na lengo lake ni kusikiliza kero na malalamiko yamigogoro ardhi ambayo ipo kwa wananchi”

“Naomba wananchi wasikilizwe mkoa mzima na kisha nipate taarifa za utatuzi wa migogoro iliyosikilizwa na baadae tukomeshe migogoro yote” amesema Mtanda.

Amesema wananchi wametangaziwa kliniki hiyo lakini walojitokeza ni wachache na matokeo yake wakiona ziara ya viongozi wa kitaifa husimama na kutoa malalamiko.

Amesema wananchi wanapaswa kuitumia fursa hiyo kupeleka kero zao na kuahidi kuzimaliza kwa namna zilivyopokelewa.

Kamishina Msaidizi wa ardhi mkoa wa Mara Joseph Batinamani amesema imeandaliwa “data” kwaajili ya kusikiliza na kupokea migogoro yote itakayotolewa ili kuepuka migogoro kutojirudia

Amesema wakiwa manispaa ya Musoma watasikiliza kero kwa Siku 5 na baadae kuhamia katika maeneo mengine ya mkoa wa Mara mkuu wa mkoa

Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wameishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia ofisi ya Kamishina Msaidizi wa ardhi kwa namna alivyoamua kumaliza migogoro ya ardhi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!