Home Biashara DC MGENI ATEMBELEA WAFANYABIASHARA, AHIMIZA MATUMIZI YA MASHINE YA EFD

DC MGENI ATEMBELEA WAFANYABIASHARA, AHIMIZA MATUMIZI YA MASHINE YA EFD

Ashrack Miraji Same kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Wilaya ya Same Bw. Eliapenda Mwanri mara baada ya kumaliza ziara yake ya kuhamasisha matumizi ya mashine za EFD kwa Wafanyabiashara Wilayani humo.

Akizungumza baada ya ziara hiyo,Mkuu wa Wilaya alitoa mwezi mmoja kwa Wafanyabiashara wote wanaopaswa kuwa na mashine za EFD wanunue mashine hizo ili waweze kulipa Kodi stahili.

“Lengo la ziara hii ni kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali hayapotei,kila mfanyabiashara alipe Kodi stahili ya Serikali ili kwa pamoja tuijenge nchi yetu” alisema Mkuu huyo.

Akizungumzia ziara hiyo Meneja wa TRA Wilaya ya Same Bw.Mwanri alisema Wilaya hiyo ina jumla ya Wafanyabiashara 1,300 waliosajiliwa TRA ambapo alisema Kati yao ni wafanyabiashara 180 ndio wanaotumia mashine za EFD.

Wapo baadhi ya Wafanyabiashara ambao wanastahili kuwa na mashine hizo kutokana na mauzo yao na hawa tayari tumeshawaandikia barua za kuwataka kununua mashine” alisema Meneja huyo.

Previous articleJELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MWANAFUNZI NA KUMSABABISHIA UJAUZITO
Next articleRC MTANDA ATAKA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA KLINIKI YA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here