Home Kitaifa RC MAKALLA: MAONYESHO YA 46 YA SABASABA 2022 YAMEFANA

RC MAKALLA: MAONYESHO YA 46 YA SABASABA 2022 YAMEFANA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Sera nzuri na mwelekeo Bora alioonyesha Rais Samia Suluhu Hassan kuitangaza Nchi kimataifa hususani Royal tour vimechagiza Maonyesho ya 46 ya sabasaba kuwa na mwamko mkubwa na ushiriki wa Makampuni mengi kutoka ndani na nje ya Nchi.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea Maonyesho hayo ambapo amefurahi kuona zaidi ya Nchi 22 zikishiriki Maonyesho hayo na Kampuni za 3,200 za Ndani 180 kutoka nje ya Nchi.

Aidha RC Makalla ameipongeza Tan trade kwa kuratibu vizuri Maonyesho hayo na kutoa wito kwa Wananchi kutembelea Maonyesho hayo ili kujionea ubunifu na bidhaa mbalimbali.

Pamoja na hayo RC Makalla amepongeza pia ubunifu wa kuanzisha route za Usafiri wa Mabasi ya mwendokasi mapaka kwenye Viwanja hivyo jambo linalorahisisha huduma ya usafiri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!