Home Kitaifa RAIS SAMIA AWASILI KAGERA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU 2

RAIS SAMIA AWASILI KAGERA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU 2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Bukoba Mkoani Kagera. Leo Oktoba 13, 2022

Mheshimiwa Rais atakuwa na ziara ya Kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera ambapo atatembelea na kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuzindua Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera.

Pia, Rais Samia atashiriki Maadhimisho ya Kilele cha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru 2022 yatakayofanyika tarehe 14 Oktoba 2022 katika uwanja wa Kaitaba – Bukoba.. (Picha na Eliud Rwechungura)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!