Home Kitaifa LATRA YAISHAURI TRC KULINDA MIUNDOMBINU YAKE ILI KUZUIA AJALI

LATRA YAISHAURI TRC KULINDA MIUNDOMBINU YAKE ILI KUZUIA AJALI

Magrethy Katengu

Maamlaka ya Udhibiti wa usafiri wa ardhini (LATRA) imelitaka shirika la Reli Nchini ( TRC) kuhakikisha linalinda usalama wa wananchi kwenye miundombinu ya reli ili kusaidia kupunguza ajali zinazotokea kupitia watu kukatiza njia za treni bila kuwa na tahadhari

Rai hiyo ilitolewa Jijini Dar es salaam na Kaimu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi LTRA Henry Bantu katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya usalama wa reli iliyojumuisha nchi wanachama wa SADC chini ya umoja wa vyama vya reli kusini mwa afrika (SARA South African Railway Association) inayoadhimishwa kila mwaka oktoba 10 na mwaka huu imekuja na kaulimbiu isemayo “Chukua tahadhali,Treni zina mwendo wa haraka,Ni hatari” .

Hivyo alisihi shirika hilo kuzingatia usalama wa wananchi katika maeneo ya miundombinu ya reli kwa kutoa elimu stahiki kwa mijini na vijijini ili waweze kufahamu alama mbalimbali za usalama zilizowekwa kwenye miundombinu ya reli hali inayoweza kusaidia kuepukana na ajali za treni.

Bantu alisema kuwa shirika hilo liweke kitengo maalumu kitakachoshughulika na ulinzi na usalama ,miundombinu ya reli,abiria,pamoja na watumiaji wengine wa reli huku sehemu isiyo na ulazima watu kukatiza kuweka uzio kwani kumekuwa na matukio ya vifo vya ajali ya watu na wanyama kwa kupita njia hiyo.

“TRC iweke baadhi ya alama,ishara,na mambo muhimu ambapo mtumiaji wa reli anapaswa kuzingatia ili kuangalia kabla ya kuvuka au kupita hakumbani na adha yeyote ya kupata ajali na kumsababishia kifo ama majeraha”alisema Bantu

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la reli Tanzania( TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa aliziomba halmashauri nchini kuwa na utaratibu wa kuishirikisha TRC kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuweza kuepusha muingiliano wa miradi kati ya TRC na Halmadhauri hizo katika baadhi ya maeneo.

Kadogosa alisema kuwa katika maendeleo ya sekta ya reli nchini ,serikali imeweka fedha nyingi kwenye ukarabati na ujenzi wa miundombinu mipya ya reli ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa SGR ili kuhakikisha usalama wa miundombinu ya reli kwa watumiaji ni lazima kuwepo kwa mikakati madhubuti ya kuhakikisha jamii inapata elimu ya usalama wa reli.

Hata hivyo aliwashauti wananchi katika makundi tofautitofauti ikiwemo wafugaji wanaochunga mifugo yao katika maeneo ya njia ya reli kuacha shughuli hizo za ufugaji katika maeneo hayo ili kuepusha ajali ambazo sio za lazima.

“Mlio na tabia ya kupiga picha katika njia za reli,kuegesha magari katika njia za reli,manaosikiliza simu nakuweka visikiliza simu masikioni,mnaotembea,mnnaokaa,mnaocheza na wale wanaoweka vitu vizito kwenye reli acheni mara moja ajali haiji kwa kupiga hodi lazima kuwe na sababu”alisema Kadogosa

Kadogosa ameongeza kuwa tayari ujenzi wa SGR kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro umekamilika kwa asilimia mia moja hivyo kwa sasa wapo katika majaribio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!