Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian tarehe 22.07.2022 amefungua kikao cha robo mwaka cha kujadili takwimu za UKIMWI na chanjo ya UVIKO-19 kwa timu ya Afya ya Mkoa, timu za Afya za Halmashauri 8 za Mkoa wa Tabora na Wadau wa Afya ( MDH)
Wakati wa ufunguzi, Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo na maelekezo ya kusimamia utoaji wa Huduma za Afya vizuri ili kuendelea kuboresha Afya za wananchi wa Mkoa wa Tabora.
Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa vyeti vya pongezi kwa wadau wa MDH na Halmashauri za Mkoa wa Tabora kwa kufanya vizuri katika chanjo ya UVIKO-19 na kufanya Mkoa wa Tabora kuwa wa kwanza Kitaifa.