Home Kitaifa KONGAMANO LA TAASISI YA IET KUFANYIKA DISEMBA 1 HADI 3 AICC

KONGAMANO LA TAASISI YA IET KUFANYIKA DISEMBA 1 HADI 3 AICC

Na. Magreth Mbinga

Chama cha Wahandisi Tanzania(IET) kimeandaa kungamano la 13 la Kimataifa na Mkutano wa mwaka wa wanachama ambapo unatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Taarifa hiyo imetolewa na Mjumbe la Baraza la Taasisi ya Wahandisi Tanzania(IET) Mhandisi Makulilo Kassera katika Mkutano na wahandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa wananchama na kualika wadau kushiriki Mkutano huo wa mwaka na kongamano.

Mpaka sasa taasisi inakisiwa kuwa na jumla ya wanachama 4,644 ,asilimia 30 Ni wahandishi waandamizi ,asilimia 50 ni Wahandisi wahitimu , fellow asilimia 2,mafundi asilimia 18″amesema Mhandisi Kassera.

Pia Mhandisi Kassera amesema matarajio ya Taasisi ni kwamba jamii ya kihandisi Tanzania itakuwa mshiriki wa utatuzi wa athari za tabia ya Nchi wanazo taarifa za mikutano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa juu ya athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi na mipango mikakati ambayo imeadhimiwa na mikutano hiyo.

Tunampongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa msimamo wake na kuwahimiza wasaidizi wake hususa ni Waziri anayehusika na mazingira azingatie mipango ya kuinusuru Nchi kutokana na athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi”amesema Mhandisi Kassera.

Sanjari na hayo Mhandisi Kassera amewakaribisha wadau wote wa sekta ya uhandisi ili waweze kushiriki katika kongamano na kutoa wito kwa Wahandisi na mafundi ambao ambao bado hawajajiunga na taasisi wsjiunge na kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yao ya www.iet.or.tz .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!