Home Kitaifa MIKAKATI YA KUKABILIANA NA TATIZO LA UMEME YAANIKWA

MIKAKATI YA KUKABILIANA NA TATIZO LA UMEME YAANIKWA

Na. Magreth Mbinga

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limesema kuwa sababu zinazochangia kupungua kwa kiwango cha umeme ni ukame ambao umepunguza kina cha maji kwenye vyanzo vya uzalishaji umeme na matengenezo ya mitambo.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Maharage Chande amesema Upungufu wa umeme kwa siku ni megawati 300 mpaka 350 jambo ambalo limesababisha mgao wa umeme ukizingatia kuwa kipindi hiki ni miezi ya joto hivyo umeme unatumika kwa wingi.

Mambo yanayosababisha upungufu kwenye gredi ya Taifa kwa sasa ni ukame kwani vituo vingi vya kuzalisha umeme vinatumia maji ikiwemo bwawa la kihansi megawati 180 likiiwa limejaa ila sasa linazalisha megawati 17 tu hivyo kupoteza megawati 163, kituo cha Pangani megawati 68 sasa kimezimwa kabisa hivyo kupoteza megawati 68 bwawa la mtera megawsti 80 na kinazalisha 68 tu” Amesema Mkurugenzi Chande.

Aidha ametaja sababu ya pili ya upungufu ni matengenezo ya mitambo ambapo vituo vilivyopo kwenye matengenezo ni kituo cha Hale, Ubungo na Kidato.

Hata hivyo amesema juhudi za muda mfupi zinazofanywa na shirika ili kupunguza tatizo la upungufu wa umeme ni kuelekeza nguvu kwenye vituo vya gesi ikiwemo kituo cha ubungo 3 ambacho wamerekebisha mitambo ili kurejesha megawati kwenye mfumo.

Kituo cha Kidato kina mashine ya megawati 50 haifanyi kazi ipo kwenye matengenezo ikikamilika itaongeza kiwango cha umeme, upanuzi wa Kinyerezi one ambapo hadi mwisho wa mwezi kitakamilika na umeme uingie kwenye mfumo ambapo tatizo la umeme litapungua kutoka na megawati 300 hadi 350 na kufikia megawati 130 hadi 70” Amesema Mkurugenzi Chande.

Sambamba na hayo amesema juhudi za muda mrefu kwa kipindi cha miezi 18 ni kuhakikisha kuwa bwawa la umeme la Julius Nyerere linakamilika ambapo litaondoa kabisa adha ya umeme Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!