Na Magreth Mbinga
Kata ya Mikocheni leo Novemba 5,2022 imezindua wiki ya maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza Nchini Tanzania ambayo yanaenda sanjari na upimaji wa afya bure maarufu kama AFYA CHEK ambayo itasaidia wananchi kufanya uchunguzi wa afya ndani ya siku saba kuelekea kilele chake Novemba 12,2022.
Akizungumza katika ufunguzi huo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa TPDC katika Kata hiyo ya Mikocheni Ndugu Ramadhani Hashim amesema Kata ya Mikocheni wamezindua katika Zahanati ya JS BABHRA ambapo Wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao bila malipo.
Ndugu Ramadhani amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan sambamba na Diwani wa Kata hiyo Eng Hussein Iddy Nzenzely kwa kufanikisha zoezi hilo kwani ni ishara ya kujali na kuwathamini Wananchi .
Aidha Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo ya JS BABHRA Dkt. zahanati hiyo inaungana na vituo vyote vya afya Nchini kutoa huduma katika maadhimisho hayo na kusema kuwa magibjwa yasiyo ambikiza ni kama sukari, shinikizo la damu[pressure], magonjwa yote yanayotokana na lishe duni na ugonjwa wa moyo.