Home Michezo CRDB TAIFA CUP YAANZA KURINDIMA TANGA

CRDB TAIFA CUP YAANZA KURINDIMA TANGA

Na. BONIFACE GIDEON, TANGA

Mashindano ya Basketball Nchini yanayodhaminiwa na Benki ya CRDB (CRDB TAIFA CUP) yamezinduliwa Jana na Novemba 4 na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omar Mgumba hapa mkoani Tanga katika Viwanja vya Michezo Mamlaka ya Bandari Tanzania Maarufu kama Habours Club .

Jumla ya Timu 32 zitapapatuana kupata Bingwa kwakila upande ambapo upande wa Wanaume kutakuwa na Timu 16 na Wanawake Watakuwa na Timu 16 ambapo zawadi zitakuwa sawa kwa wote.

Ufunguzi huo uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omar Mgumba pamoja na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Tanga pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Tanga ambapo Mgumba aliwataka Wanamichezo kulinda Afya zao ili wawe timamu muda wote wa Ujana wao,

Nimewaona hapa Wachezaji wote ni Vijana wadogo Sana na Wengi wenu Bado mpo kwenye masomo, niwasihi Sana mlinde Afya zenu msiingize kwenye mambo ambayo yanaweza kuharibu Afya zenu ikiwamo Matumizi ya Dawa za Kulevya lakini pia na ngono Uzembe hivyo mjilinde Sana na vitu hivyo ili muwe na Afya Bora Mana Ujana ni kuwa na Afya Bora” Alisisitiza RC Mgumba

Kwa upande wake Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa alisema kuwa dhamira yao ni kuona mchezo huo unazidi kukua hapa nchini ambao utaendana sambamba na maendeleo ya vijana wanaochezea mchezo huo hatua ambayo itakwenda kupunguza wimbi la vijana nchini wasio na kazi za kudumu ambapo wengi wao wamekuwa wakijiingiza katika makundi hatarishi

Moja kati ya malengo ya CRDB Taifa Cup ni kuleta hamasa ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanaocheza katika mikoa yote hapa nchini”

Alisema kuwa mbali na mchango wanaoutoa kupitia michezo wamekuwa ni wadua wakubwa wa maendeleo pia ambapo kwa kipindi cha mwaka jana benk hiyo iliweza kutoa shilingi Million 10 kwaajili ya vifaa vya ujenzi wa shule nne zilizopo wilaya ya Kilindi mkoani hapa, wakitoa pia million 40 kwaajili ya ujenzi wa madarasa na ofisi ya walimu katika shule maalumu Chuda iliyopo jijini Tanga.

Sisi CRDB ni wadau wakubwa wa maendeleo mkoani Tanga na hata kanda nzima ya Kaskazini kwa ujumla wake, hapa Tanga kwa mwaka jana benki ilitoa vifaa vya ujenzi kwaali ya ujenzi wa shule iliyopo Kilindi vyenye thamani ya shilingi Million 10 kama moja ya muendelezo wa mipango ya benki katika sera yake ya kuwekeza katika jamii, pia benki ilitoa million 40 kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu katika shule maalumu ya Chuda ambayo yatakwenda kuzinduliwa mwaka huu”, alisema Chiku.

Vilevile mwaka 2022 tulitoa ufadhili wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za msingi za wilaya ya Tanga mjini hii inaendana kabisa na ajenda yetu ya kuwezesha vijana kufikia ndoto zao Kama moja ya vipaumbele ya benki ya CRDB” aliongeza.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania

Rwehabura Barongo kadiri siku zinavyokwenda maendeleo ya mpira wa Kikapu yanazidi kuonekana na kuleta Mapinduzi makubwa kwa maendeleo ya wachezaji na Chama hicho hatua ambayo inachagizwa kwa kiasi kikubwa na wadau mabalimbali wanaojitoa katika kusaidia mchezo huo wakiwemo wadhamini wakubwa wa ligi hiyo ngazi ya Taifa benki ya CRDB.

Sasa hivi Tanzania hii huwezi kuzungumzia basketball bila kutaja benki ya CRDB na hii fursa imekuwa sio ya wadau wa Tanzania pekee bali hata kimataifa , tumepata barua kutoka Giant of Afrika wataleta skauti wao kuja kuangalia vipaji vya mpira wa Kikapu Tanzania haya ni kutokana na matokeo chanya ya ushirikiano wa mikoa yote inayoshiriki ambao walikuwa na ligi za mkoa walizofanya kwa wakati na muda sahihi” alisema Barongo.

Uzinduzi wa ligi hiyo amabao umefanyika jana November 4 itaendelea hadi November 12 ikiwa ni Mara ya kwanza kufanyika mkoani Tanga na mara ya tatu kuchezwa kwa ligi hiyo hapa nchini ikifanyika kwa Mara mbili mfululizo mkoani Dodoma bingwa kwa upande wa wanawake Wanaume akitarajiwa kuondoka na kitita cha shilingi million 10, huku washindi wa pili wqo wakijinyakulia shilingi million 5 uwkezaji ambao ni mkubwa ambao umefanywa na benki ya CRDB.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!