Home Burudani TAMASHA LA MUZIKI WA ACCESS AFRIKA

TAMASHA LA MUZIKI WA ACCESS AFRIKA

Na Mercy Maimu

Katika kuelekea maazimisho ya Mkutano wa Muziki wa Access ulioandaliwa na Taasisi ya Music Africa utakaofanyika Novemba 24 -26,2022 Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni sanaa na michezo Dkt Hassan Abbas amewataka wasanii kuhudhuria mkutano huo kwani utatambulisha vipaji vyao na kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa Leo 4 Nov ,2022 na Dkt Hassan Abbas wakati akizungumza na waandishi wa habari.Aidha amesema serikali na Wadau wamewekeza na wamechukulia tamasha Hilo kiukubwa na uzito sana. Pia kupitia Royal Tour imesaidia Wizara ya utamaduni na sanaa kupata fursa mbalimbali kimataifa.”

” Kabla ya Royal Tour Nchi yetu ilikua ya 12 kwenye kuandaa na mashindano ya Miss &Mister Deaf ila baada ya Royal Tour tumepewa nafasi ya kuandaa na kuongoza mashindano hayo na kuibuka kidedea kupata Mrembo wa kwanza duniani. Tulifanya Royal Tour Nchi yetu kuwa ya Tisa(9) duniani kushiriki programu kubwa sana ya kuitangaza Nchi yetu duniani”. Amesema Abbas

Naye Mkurugenzi wa Music in Africa Foundation Eddie Hatitye amesema wanamuziki wengi wakufa wakiwa masikini kutokana na kutopata ufikiaji mzuri katika kazi zao na kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu Muziki na jinsi ya kujipatia kipato kupitia kipaji Chao.

Wasanii wengi ni maarufu lakini ukiwafuatilia kuindani maisha wanayoishi ni ya kimasikini sana na wengine hata kufariki wakiwa Bado na hali duni za maisha. Hii ni kutokana na kutokufanya musiki kama biashara na Ajira”.amesema Eddie

Kwa upande wake Farid Kubanda (Fid Q)amewataka wanamuziki kutumia tamasha hilo kama njia ya kupata marafiki wengi na kujiunganisha nao ili kukuza muziki wa Taifa letu na kufanya Muziki kama Ajira sio kuimba kwa kujifurahisha.

Ameongeza kwa kusema Tamasha Hilo litafanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere na litakuwa na Mikutano,Waimbaji wa ndani na nje ya Nchi watahudumia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!