Home Kitaifa JOKATE AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAMA ALIYEJIFUNGUA WATOTO WANNE

JOKATE AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAMA ALIYEJIFUNGUA WATOTO WANNE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo leo amekabidhi Pikipiki aina ya Boxer kwa Mwanamama Fatuma ambaye alijifungua watoto wanne kwa wakati mmoja.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema leo mara baada ya kukabidhi Pikipiki hiyo DC Jokate amesema kuwa ameamua kumkabidhi chombo hicho hili kumpunguzia Mama huyo makali ya maisha ya kulea watoto hao

Mwaka huu mwezi wa pili alijifungua wtoto wanne kwa wakati lakini lengo lake lilikuwa kujifungua mtoto mmoja hivyo baada ya kujifungua tuliweza kumpa msaada wa awali wa nepi na nguo lakini sasa lengo la ofisi yangu ni kumpatia kifaa ambacho kitaweza kumsadia kujipatia kipato cha kila siku hili aweze kununua maziwa ya watoto” amesema DC Jokate.

Ametaja kuwa mara baada ya kujifungua watoto Mama huyo ameweza kusimama shughuli zake zote hivyo awezi kutembea kwenda kujitafutia kipato wala kufanya shughuli yoyote.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ametoa Maelekezo kwa Mtendaji kata wa Mtaa anakotekea Mama huyo kuhakikisha anampatia Dereva ambaye ni Mwaminifu atakayefanya kazi na kumpatia mama huyo pesa hili aweze kusaidika na malezi ya mtoto huyo .

kwa upande wake Bi Fatuma aliweza Kumshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuweza kumpatia msaada huo kwani utaweza kumsaidia sana katika kuweza kupata chakula cha watoto hao.

Bi Fatuma ambaye ni Mama wa Watoto Saba aliweza kujifungua Mtoto Mmoja katika Uzao wa Kwanza na watoto Mapacha katika uzao wake wa Pili na Katika uzao wake huu wa tatu ameweza kujifungua watoto hao wanne kwa wakati mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!