Na Magreth Mbinga
Maadhimisho ya siku ya uzazi wa mpango ni muhimu sana kwa Serikali sababu maisha ni kujipanga kutokana na malengo uliyojiwekea kwahiyo elimu ya uzazi wa mpango izingatiwe ili kama jamii tuweze kujipanga vizuri zaidi watoto tunaowapata wazaliwe kwenye mazingira bora na mazuri .
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh Joketi Mwegelo katika hafla ya siku ya uzazi wa mpango Duniani iliyoandaliwa na DKT Tanzania na kufanyika katika Hospitali ya Mbagala rangi tatu iliyopo Wilayani humo Jijini Dar es Salaam.
“Tunachangamoto kubwa ya watoto kuzaliwa katika ndoa zilizovunjika mtoto anazaliwa baba hataki kushika majukumu yake mama analea pekeyake au motto anazaliwa wazazi hawana muda wa kulea yule mtoto lakini Elimu hii ya uzazi wa mpango wakiizingatia wataweza kuwa na utulivu wa akili” amesema Mh Joketi.
Pia amewataka wazazi kuwalea watoto katika maadili mazuri ili kutengeneza jamii ya bora na kuepukana na changamoto ya watoto kuwa na makundi ya ajabu kama panya road ambapo hao ni watoto wanaotoka kwenye jamii .
Aidha Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeka Dk Irene Haule amesema katika kuadhimisha siku ya uzazi wa mpango wamepata
fursa ya kuona wazazi walio jifingua kawaida na wa oparesheni ndani ya Hospitali ya Mbagala rangi tatu .
“Kama wote tunavyojua kwamba uzazi wa mpango ni muhimu sana kwa maana ya maisha ya mtoto na mama kuwa salama pia inawaongezea wazazi kuweza kuwa na uwezo mzuri wa kupata familia bora maana ya malezi na makuzi na mwisho tuwe na jamii ambayo inatija kwa Taifa letu” amesema Dk Irene.
Sanjari na hayo Meneja Masoko DKT International Tanzania Dk Deogratius Kithama ambayo wameandaa hafla hiyo na kukabidhi zawadi kwa wazazi hospitali hapo amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa kuitikia with kwa kuhudhulia hafla hoyo.
“Sisi kama DKT Tanzania tukisema jipange iwe ni mwanzo wa kampeni ya kuhamasisha jamii kwa ujumla umuhimu wa kupanga uzazi ikiwa ni moja ya viashiria vya kwamba mtu atakuwa na uchumi kiasi gani ili ajue idadi wa watoto atakao mudu kuwalea na kuwapatia mahitaji muhimu ” amesema Dk Deogratius.
Vilevile Dk Elizabeth Mahagi ambae yupo kitengo cha uzazi wa mpango amesema muitikio ni mkubwa katika hospitali hiyo ambapo watu wengi wanajitokeza hasa njia ya kipandikizi ndio inaongoza zaidi maana watu wengi wanaona ni rahisi .