Home Kitaifa BASHUNGWA AONYA HALMASHAURI ZINAZOVUKA NA FEDHA MWAKA MWINGINE.

BASHUNGWA AONYA HALMASHAURI ZINAZOVUKA NA FEDHA MWAKA MWINGINE.

Angela Msimbira MANYARA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amepiga marufuku Halmashauri zote nchini kuacha tabia ya kuvuka na fedha mwaka mwingine wa fedha (Bakaa) na kuzielekeza kwenye matumizi yasiyofaa.

Bashungwa ameyasema hayo leo Septemba 24, 2022 alipokuwa akikagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya Lalaji iliyopo katika Kata ya Lalaji, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’, mkoani Manyara.

Amesema kuwa kumeibuka tabia ya Halmashauri kuvuka na fedha mwaka mwingine wa fedha na kuzielekeza kwenye matumizi yasiyofaa ikiwamo safari zisizo kuwa na tija badala ya kuzielekeza kwenye utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.

Amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafanya tathmini ya fedha zote za bakaa ili ziende kwenye kutekeleza miradi ya maendeleo na sio matumizi mwingine yasiyofaa.

Hizi fedha za bakaa zipelekwe kwenye kutekeleza miradi ya maendeleo kama ujenzi wa madarasa, mabweni, mabwalo, vituo vya afya, na ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuwasaidiaa wananchi,”amesema.

Ameongeza kuwa Wananchi wanakiu ya kupata maendeleo hawatafurahi kuona tunazunguka nchi nzima kwa kutumia bakaa ya fedha ambayo ilitakiwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Amemuagiza Kaimu Katibu Mkuu Dkt.Charles Msonde kuhakikisha anafanya uchambuzi wa fedha za bakaa zilizobaki katika halmashauri na kutoa taarifa ya matumizi ya fedha zilizobaki kama bakaa na matumizi yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!