Home Kitaifa RSA YAMSHUKURU RAIS SAMIA FILAMU YA ROYAL TOUR KULETA NEEMA SEKTA...

RSA YAMSHUKURU RAIS SAMIA FILAMU YA ROYAL TOUR KULETA NEEMA SEKTA YA UTALII NCHINI.

Na.Elizabeth John,Njombe

Mkurugenzi wa kampuni ya RSA inayojihusisha na utengenezaji magari ya utalii Harveer Bhamra,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya Royal Tour ambayo imeleta mafanikio katika kukuza sekta ya utalii nchini.

Ameyasema hayo leo wakati uzinduzi wa mkakati wa kutangaza utalii kusini,Bhamra amesema kuwa baada ya kutoka kwenye covid 19 watalii wameanza kuja kwa wingi.

“Ukiangalia ndege zinashuka zimejaa,ukienda Serengeti,Ngorongoro kila mahali tunaona watu wanakuja kwa wingi Juzi hata kuingia getini magari yamejaa kwa wingi sana”amesema Bhamra.

Amesema magari wanayotengeneza wanapata wateja tofauti tofauti ambao wananunua magari hayo ya kisasa ili kuendeleza utalii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here