Home Burudani DKT.ABBASI:TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA MUSIC IN AFRICA

DKT.ABBASI:TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA MUSIC IN AFRICA

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi leo Septemba 15, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Taasisi ya Music in Africa ambao kwa kushirikiana na Wizara pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wanaandaa Mkutano mkubwa wa sekta ya muziki Afrika (Music in Africa Conference).

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Bodi ya Filamu zilizopo Barabara ya Kivukoni, Utumishi jijini Dar es salaam, ambapo Dkt. Abbasi amesema, Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaofanyika Novemba 24-26, 2022.

“Mkutano huo unatarajiwa kuleta fursa mbalimbali za kukutana na wadau mbalimbali wa muziki kutoka Afrika na duniani kwa ujumla ambapo wasanii mbalimbali watapata nafasi ya kutumbuiza” amesema Dkt. Abbasi.

Amewataka Wasanii na wadau wa muziki nchini kuthibitisha ushiriki wao kupitia mtandao wa @musicinafricaofficial

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!