Na Magreyn Katengu
Shirika la ndege Tanzania (ATCL) linatarajia kuongeza idadi ya safari kutoka safari 4 hadi kufikia 5 kwa wiki ifikapo mwezi Octoba mwaka huu ili kukabiliana changamoto yaa ongezeko la abiria.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi wakati akitoa taarifa yake, kuhusu ziara ya kikazi aliyoifanya jijini Mumbai , China ambapo alifanikiwa kukutana na wadau mbalimbali yakiwemo Makampuni makubwa ya uzalishaji na usambazaji wa Madawa, uuzaji wa tiketi na ya Ndege pia Uongozi wa hospitali mbili (2) kubwa jijini Mumbai mwaka 2019, Air Tanzania iliongeza mtandao wake wa safari kwa kuingia kwenye soko la Mumbai, India na walianza na safari moja kwa wiki kwa kutumia ndege hizo za abiria kulihudumia soko hilo na sasa wanasafari nne (4)
kwa wiki.
Mhandisi Matindi alisema Kwa kutumia ndege zao za abiria walifanikiwa kumiliki asilimia 80 ya abiria wote wanaosafiri kati ya Tanzania na Mumbai sawa na wastani wa abiria Zaidi ya elfu 66 kwa mwaka.
“Ukweli ni kwamba idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na abiria wote wanaosafiri nje ya nchi hiyo kila mwaka hususan watalii, tulifanikiwa kumiliki asilimia 80 ya abiria wote wanaosafiri kati ya Tanzania na Mumbai kutokana na ubora wa huduma kupitia aina ya ndege Boeing 787- 8 Dreamliner (ndege za kisasa, zenye utulivu angani, nafasi kubwa na uwezo wa kuwafanya wasafiri wajisikie ufahari, uwezo wa Kampuni katika kumudu soko naAbiria wanaosafiri na ndege zetu wameendelea kufurahia huduma ya mtandao “Wifi” angani, vyakula vya asili kwa wasafiri pamoja na viburudisho.” Alisema Matindi
Pia Matindi amefafanua kuwa Ndege mpya ya kisasa ya mizigo Boeing 767- 300F kutoka shirika la Ndege Tanzania (ATCL), imeanza safari zake na imeendelea kusafirisha mizigo ya aina mbalimbali ikiwem biidhaa zinazoharibika kwa muda mfupi, Bidhaa za kawaida na Bidhaa zenye uhitaji wa udhibiti wa hali ya hewa ya kiwango maalum kama vile madawa.
Mhandisi Matindi amesema Uwepo wa ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 54 kwa mara moja
imewezesha Kampuni ya Glenmark Pharmaceutical, mojawapo ya makampuni makubwa ya utengenezaji wa madawa ya binadamu nchini India, kukubali kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usambazaji wa madawa ya Kampuni hiyo barani Afrika kwa kutumia ndege zetu.
Aidha alisema hadi sasa kampuni kubwa zimekubali kuingia nao makubaliano lengo ikiwa ni kuendelea kuboresha utoaji wa huduma”MakeMyTrip inayohusika na uuzaji wa tiketi za ndege na uwezeshaji wa safari za kitalii nchini humo Make MyTrip ambayo inatumia tovuti yake kuuza tiketi za Air ndani ya Tanzania na nje ya India pia imekubali kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia tovuti hiyo.
Pia Matindi amesema wamefanikiwa pia kuanzisha mazungumzo ya mashirikiano yakibiashara ya kubebeana abiria (Interline Agreement) na Kampuni ya Ndege ya Vistara.
“Kampuni hii ina mtandao mkubwa kwa safari za ndani nchini India hivyo itarahisisha uunganishaji wa safari za ndani kwa abiria wa ATCL wanapofika jijini Mumbai.”
Alisema wameanzisha mazungumzo na hospitali mbili (2) zilizopo jijini Mumbai kwa ajili ya kuingia makubaliano ya kibiashara ambapo makubaliano
hayo yatawezesha wagonjwa wanaotoka Tanzania kupata punguzo la gharama za matibabu wanapotumia ndege zetu.
“Tayari tuna mahusiano ya kibiashara na hospitali ya Kokilaben iliyoko Mumbai ambapo wasafiri wanaotumia ndege zetu hupata punguzo la
gharama za matibabu wanapotibiwa katika hospitali hiyo.”
Kadhalika Mhandisi Matindi amesema katika ziara hiyo alifanikiwa kukutana na Balozi Anisa Mbega,
Balozi wa Tanzania nchini India, na kupongeza kwa juhudi anazozifanya kutangaza fursa na vivutio vilivyopo Tanzania ikiwemo maonesho nchini India ambapo ATCL wameshiriki kwenye baadhi ya maonesho hayo.
Kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa ATCL, Mhandisi Matindi amesema wameendelea kuboresha utoaji wa huduma, kununua ndege mpya za kisasa na kupanua mtandao wa safari ili kuendana na kasi ya mahitaji halisi ya soko la Anga.
Aidha, Kwa sasa wana ndege mpya
Masafa ya mbali tatu (3) – Boeing 787-8 (2) na Boeing 767-300F (1), Masafa ya kati nne (4) – Airbus 220-300 na Masafa mafupi sita (6) – Q400 (5).








