- YAAHIDI KULETA MGOMBEA SAFI KATA YA BUSEGWE
Na Shomari Binda-Butiama
CHAMA cha Mapinduzi “CCM” kimetajwa kuendelea kushika dola na kuiongoza Tanzania kutokana na kazi nzuri iliyofanya kwa kipindi cha miaka 47.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake “UWT” mkoa wa Mara Nancy Msafiri kwenye sherehe za miaka 47 ya CCM wilayani Butiama.
Amesema miaka 47 iliyopita hadi leo yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana hivyo CCM ina kila sababu ya kuendelea kushika dola.
Nancy amesema wilaya ya Butiama leo incho chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere ambacho miaka 47 iliyopita hakikuwepo na hiyo ni moja ya maendeleo yaliyopigwa.
Amesema licha ya chuo kikuu hicho zipo shule nyingi zilizo jengwa kuanzia msingi na sekondari na kutoa nafasi ya kupata elimu.
Mwenyekiti huyo amesema wananchi wanapaswa kuendelea kukiamini chama hicho na kukipa nafasi ya kuendelea kuiongoza nchi.
“Miaka 47 yapo maendeleo makubwa ambayo yamefanyika hapa nchini na hata kwenye wilaya yetu ya Butiama”
“Na kwenye kipindi hiki cha awamu ya 6 ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kasi ya maendeleo imepigwa zaidi tumpe mama mitano tena” amesema Nancy.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Butiama Marwa Siagi amesema chama kitaleta mgombea safi anayekubalika Kata ya Busegwe kwenye uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha diwani aliyekuwepo.
Amesema mgombea safi na anaye kubalika kwa wananchi anapelekea chama kutokuangaika kumnadi wakati wa kampeni.








